MATUMAINI DAFUR
24 Machi 2007Matangazo
KHARTOUM:
Mjumbe maalumu wa UM kwa Dafur, amesema ana matumaini mazuri kwamba vikundi vinavyogombana huko Dafur vyaweza vikafikia mapatano ya kuacha mapigano .Amesema vikundi vilivyokataa hapo kabla mazungumzo, sasa vitayari kujadiliana-hii ni kwa muujibu wa Radio ya Sudan ilivyoripoti hii leo.
Jan Eliasson, mjumbe maalumu wa katibu Mkuu wa UM Ki-moon aliwasili mjini Khartoum, jana usiku.Anatazamiwa kuungana na mjumbe mwenzake wa Umoja wsa Afrika Dr.salim Ahmed Salim kujaribu kufufua utaratibu wa amani huko Dafur.