Maswali matano kwa Uingereza na EU baada ya kujitoa | Matukio ya Kisiasa | DW | 25.06.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Maswali matano kwa Uingereza na EU baada ya kujitoa

Waingereza walipiga kura ya maoni Alhamis (23.06.2016)kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya. Yafuatayo ni majibu kwa maswali muhimu juu ya kitu gani kitatokea baadaye katika uhusiano kati ya Uingereza na kundi hilo la mataifa.

Euromaxx Brexit Großbritannien

Bendera ya Uingereza

Umoja wa Ulaya umo katika mshituko na unaingia katika neo ambalo bado hailijui. Hakuna mwanachama ambaye aliwahi kujitoa na kifungu cha 50 cha mkataba wa Ulaya, ambao unaweka utaratibu wa nchi kujitoa, unatoa maelezo machache.

Licha ya kuwa unatoa maelezo ya juu juu ya kisheria kwa kipindi cha miaka miwili cha kujiondoa, wengi wanaamini itachukumua muda mrefu kuweza kuweka uhusiano mpya wa kibiashara kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya na baadhi wanahofia kuwa hatua hizo zitakuwa ngumu, zitakazoleta mvurugiko wa uchumi na masuala ya Ulaya kwa pande zote.

Brexit Nigel Farage

Mwanaharakati aliyefanya kampeni ya kijitoa Nigel Farage

David Cameron alisema atajiuzulu ifikapo Oktoba mwaka huu na kumwachia mrithi wake kuwa kiongozi wa chama cha Conservative kuufahamisha Umoja wa Ulaya kwamba Uingereza inajitoa kupitia maelekezo ya kifungu cha 50.

Hali hiyo itauweka muda wa miaka miwili wa kukimbizana, na Umoja wa Ulaya wenyewe hauwezi wanaamini maafisa, kuanzisha hatua hiyo wenyewe. Baadhi katika Umoja wa Ulaya wanataka mchakato kuanza hata haraka zaidi wakati Cameron akizungumza na viongozi wa Umoja wa Ulaya katika mkutano siku ya Jumanne wiki ijayo, na wana wasiwasi juu ya taarifa kutoka kwa waliofanya kampeni ya kujitoa kwamba wangependelea kuanzisha majadiliano mapya kabla ya kufikia kifungu 50 cha kujitoa.

Infografik Brexit Wahl nach Altersgruppen Russisch

Jinsi watu walivyopiga kura kulingana na umri nchini Uingereza

Mrithi mtarajiwa

Mrithi mtarajiwa wa Cameron, Boris Johnson alisema haoni sababu yoyote kuanza mchakato huo na kwamba hakuna kinachohitajika kubadilika katika kipindi hiki kifupi.

Makubaliano aliyoyapata Cameron na viongozi wa Umoja wa Ulaya mwezi Februari kudhibiti uhamiaji, kulinda maslahi ya kifedha ya Uingereza kutoka kanda ya euro na kujitoa kutoka katika "umoja wa karibu zaidi" yamekufa kutokana na matokeo ya kura hiyo ya maoni na viongozi wa Umoja wa Ulaya wameondoa uwezekano wa mazungumzo mapya katika utaratibu mpya wa uanachama wa Uingereza katika Umoja wa Ulaya "kuondoka maana yake kuondoka."

Wengi wanataka kuvunjika kwa haraka kwa ndoa katika muda wa miaka miwili, wakati majadiliano kuhusiana na masharti kwa ajili ya hali ya baadaye ya uhusiano wa mbali huenda yakachukua muda mrefu zaidi.

Kipindi cha mpito

Hata hivyo, Ujerumani, hususan ina nia ya kuona utaratibu mzuri wa kipindi cha mpito kuwa na uwezekano wa uhusiano mpya.

Brexit Angela Merkel

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akilihutubia taifa baada ya kura nchini Uingereza

Hii itahusisha majadiliano mapya ya kifungu 50, ambacho mkataba unasema , kinapaswa "kuchukuliwa maanani" kuhusiana na uhusiano kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya, ukirefushwa kupindukia miaka miwili ili kuruhusu muda zaidi wa kupatikana makubaliano mapana zaidi.

Urefushwaji wa aina hiyo unahitaji ridhaa ya mataifa 28 wanachama, na kufikia kauli hiyo ya pamoja inaweza kuwa na matatizo.

Pamoja na hayo, wanasheria wa Umoja wa Ulaya na wanasiasa wanatambulika kwa kutokuwa wakweli. Afisa mmoja wa Umoja wa Ulaya alisema kwamba mkataba wa kuvunja ndoa unahitaji wingi mdogo tu na makubaliano yanaweza kufikiwa kwa muda wa miaka miwili lakini kuanza rasmi ni baada tu ya makubaliano ya pili kuanzisha uhusiano mpya yatakapokamilika.

Brexit Reaktionen Geert Wilders

Kiongozi wa siasa za mrengo mkali wa kulia Geert Wilders wa Uholanzi akifurahia matokeo ya kura ya maoni Uingereza

Kuna idadi kubwa ya njia zilizowazi kwa Uingereza , ikiwa ni pamoja na kuendelea na matumizi ya soko la Umoja wa Ulaya katika utaratibu kama wa Uswisi na Norway, licha ya kuwa viongozi wa Umoja wa Ulaya wamesema gharama ya hali hiyo inaweza kuruhusu uhamiaji huru katika Umoja wa Ulaya na kukubali sheria nyingine za Umoja wa Ulaya ambapo wapiga kura wa Uingereza wamezikataa katika kura ya maoni.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Yusra Buwayhid

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com