Mashambulizi mengine yatokea Pwani ya Kenya | Matukio ya Afrika | DW | 08.07.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mashambulizi mengine yatokea Pwani ya Kenya

Taarifa kutoka wilaya ya Lamu iliyoko Pwani ya Kenya, zinaeleza kwamba wananchi waliojawa na woga kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara wamekuwa wakilala vichakani, wakihofia kuvamiwa ndani ya nyumba zao usiku.

Jeshi la Polisi pamoja na kikosi cha Msalaba Mwekundu wakiwa katika eneo la tukio

Jeshi la Polisi pamoja na kikosi cha Msalaba Mwekundu wakiwa katika eneo la tukio

Leo hii wakazi wa eneo la Hindi ambako watu zaidi ya 20 waliuawa katika mashambulizi ya Jumamosi iliyopita, asubuhi ya leo wamefanya maandamano makubwa na kufunga barabara inayounganisha eneo lao na Mombasa, na kutoka mahali hapo Daniel Gakuba amezungumza na Eric Kilakya, mkuu wa kituo cha Redio cha Sifa FM na kwanza alimuuliza ni nini hasa malalamiko ya wananchi hao ? Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Daniel Gakuba

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada