1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Marekani na washirika wake zadungua droni 15 za Yemen

Tatu Karema
9 Machi 2024

Waasi wa Houthi warusha droni katika Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden

https://p.dw.com/p/4dKnT
Meli ya Marekani ya  USS Carter Hall (LSD 50) ikipia katika Bahari ya Shamu mnamo Agosti 8, 2023
Meli ya Marekani ya USS Carter Hall (LSD 50) Picha: U.S. Marine Corps/abaca/picture alliance

Kamandi kuu ya jeshi la Marekani CENTCOM, imesema shambulizi hilo kubwa la Houthi, lilifanyika kabla ya alfajiri ya leo.

Muda mfupi baadaye, waasi hao wanaoungwa mkono na Iran walidai kuhusika na shambulizi hilo na kusema walirusha makombora dhidi ya meli ya kibiashara ya Marekani na droni dhidi ya meli za kivita za Marekani.

Soma pia:Bahari ya Shamu: Je, meli za kivita za EU zitawazuwia waasi wa Houthi?

CENTCOM na vikosi vya muungano wa kijeshi katika eneo hilo, zimesema mashambulizi hayo yanaibua tishio kwa meli za kibiashara, jeshi la wanamaji la Marekani na meli za muungano wa kijeshi katika kanda hiyo.

Soma pia:Wahouthi wazilenga meli za Marekani, Washington yajibu

Waasi wa Houthi wamekuwa wakizilenga meli za mizigo kwenye ujia wa Bahari ya Shamu wakisema ni kwa lengo la kuishinikiza Israel kusitisha mashambulizi yake kwenye Ukanda wa Gaza