1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Rwanda zasaini mkataba wa dola milioni 228

7 Desemba 2025

Marekani na Rwanda zimetia saini mkataba wa miaka mitano wa dola milioni 228 kwa sekta ya afya katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Haya ni kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

https://p.dw.com/p/54tz9
Afrika Rwanda, Corona
Mwanamke apokea chanjo ya COVID-19 mjini Kigali Rwanda mnamo Agosti 23, 2021Picha: Cyril Ndegeya/ Xinhua News Agency/picture alliance

Hayo ni makubaliano ya pili chini ya utaratibu mpya wa utawala wa Trump wa misaada ya nje. Wizara hiyo imesema mkataba huo na Rwanda unatoa mweleko wa kina wa kuokoa maisha, na kuimarisha mfumo wa afya wa Rwanda pamoja na kuisaidia Marekani kuwa salama.

Pia imesema chini ya makubaliano hayo ya afya, Marekani itaipa Rwanda hadi dola milioni 158 kukabiliana na Virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine ya kuambukiza .

Ufadhili huo pia utaimarisha ufuatiliaji wa magonjwa na kukabiliana na miripuko.

Wizara hiyo imeongeza kusema kwa upande wake, serikali ya Rwanda inapanga kuongeza uwekezaji wake wa afya wa ndani kwa dola milioni 70, ikichukua uwajibikaji mkubwa zaidi wa kifedha katika wakati ambapo msaada wa Marekani unaendelea kupunguzwa  hatua kwa hatua.