MAPUTO:Utoaji mimba kuhalalishwa | Habari za Ulimwengu | DW | 11.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MAPUTO:Utoaji mimba kuhalalishwa

Msumbiji inapanga kuidhinisha utoaji wa mimba kufuatia ripoti ya Wizara ya Afya inayoeleza kuwa takriban wanawake 100 wanapoteza maisha yao kila mwaka baada ya kutoa mamba katika vituo visivyo halali.

Utoaji mimba nchini humo ulipigwa marufuku kwa mara ya kwanza mwaka 1886 na kusisitizwa tena mwaka 81 miaka sita baada ya kupata uhuru wake kutoka kwa Ureno,.

Tangazo hilo limezua hisia kali kwani wakazi wengi ni wafuasi wa dini ya Kikatoliki huku makundi ya wanawake yakitoa wito wa kufanywa mabadiliko.

Kwa mujibu wa wizara ya afya asilimia 30 ya wanawake wanaopelekwa hospitali baada ya kutoa mimba katika kliniki zisizokuwa halali hupoteza maisha yao.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni WHO zinaonyesha kuwa yapata wanawake alfu 68 hufariki kila mwaka kwasababu ya kutoa mimba katika njia zisizo salama wengi wao katika mataifa yanayoendelea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com