1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaPapua New Guinea

Maporomoko ya udongo yaua mamia ya watu Papua New Guinea

26 Mei 2024

Shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM)limeongeza makadirio yake ya idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya udongo nchini Papua New Guinea hadi zaidi ya watu 670.

https://p.dw.com/p/4gI9W
Wanakijiji wakitafuta manusura baada ya kutokea maporomoko ya udongo katika kijiji cha Yambali
Wanakijiji wakitafuta manusura baada ya kutokea maporomoko ya udongo katika kijiji cha YambaliPicha: Mohamud Omer/International Organization for Migration/AP/picture alliance

Shirika la kimataifa la uhamiaji  IOM limeongeza makadirio yake ya idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya udongo nchini Papua New Guinea hadi zaidi ya watu 670.

Mkuu wa ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa katika taifa hilo la kisiwa cha bahari ya Pasifiki Kusini Serhan Aktoprak amesema idadi hiyo ya mpya ya vifo imetokana na hesabu ya maafisa katika kijiji cha Yambali na mkoa wa Enga kuwa, zaidi ya nyumba 150 zilifunikwa na maporomoko ya udongo siku ya Ijumaa.

Soma pia: Maporomoko ya udongo yauwa 100 Papua New Guinea

Makadirio ya awali ilikuwa ni nyumba 60 tu.

Mnamo siku ya Ijumaa, maafisa wa eneo hilo walieleza kuwa watu waliofariki kutokana na janga hilo walikuwa ni 100 au zaidi na kufikia leo, miili ya watu wengine watano na mguu wa mhanga wa sita imepatikana.

Serikali ya kisiwa hicho inazingatia kuomba misaada zaidi ya kibinadamu kushughulikia janga hilo.