Mapigano yasitishwa kwa muda Gaza | Matukio ya Kisiasa | DW | 17.07.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mapigano yasitishwa kwa muda Gaza

Rais Mahamud Abbas anatarajiwa kukutana na Kiongozi wa Misri Abdel Fattah al-Sisi leo hii kwa lengo la kufikisha kikomo hujuma ya operesheniya Israel iliyosababisha mauwaji makubwa katika eneo la ukanda wa Gaza.

Gaza Palästina Israel Krieg Bombardierung Zivilbevölkerung

Hali ilivyo katika eneo la Ukanda wa Gaza

Tangazo hilo lililotolewa na ofisi ya rais wa Misri linatolewa wakati Israel na kundi wapalestina la harakati za Kiislamu la Hamas zikikubaliana kusitisha mapigano kwa muda ili kuruhusu misaada ya kibinaadamu.

Hatua hii ya kusitisha mapigano kwa muda inafanyika baada ya kuwepo kwa mfululizo wa mashambulizi ya Israel, kwa kutumia maroketi katika eneo la Ukanda wa Gaza ambayo yalianza rasmi Julai nane, ambapo leo hii yanatimizia siku ya 10. Kwa mujibu wa watoa tiba katika eneo hilo mpaka sasa Wapelistina 227 wameuwawa na katika kipindi hicho hicho Muisrael mmoja aliuwawa kutokana na kombora la roketi lilivuka mpaka.

Jitihada za Misri kusitishwa mapigano

Athari za makombora ya Israel katika Ukanda wa Gaza

Watoto na wanawake wamekuwa waathirika wakubwa

Serikali ya Misri kwa mara nyingine imekuwa kitovu cha suluhu ya kidiplomasia kwa lengo lile lile la kuyafikisha kikomo mapigano hayo na hasa baada ya pendekezo lake la awali kushindwa kutokana na kutofikia muafaka wa matakwa ya upande wa Hamas.

Leo hii serikali imekutana na naibu kiongozi wa kundi la Hamas Mussa Abu Marzuq, ambae amesisitiza kuwepo mabadiliko ya mpango wa kusitishwa mapigano wa Misri, likiwemo hakikisho la kufungua mipaka ya eneo lililozingirwa la Ukanda wa Gaza. Awali Israel ilikubaliana na jitihada hizo za Misri lakini baadae ikaongeza zaidi mashambulizi yake ya anga baada ya Hamas kukataa mpango huo kwa kusema haikushauriwa.

Katika muendelezo wa kile kinachoendelea katika ardhi ya Palestia, raia leo hii wameonekana kukimbilia katika maduka na mabenki kwa lengo la kujipatia mahitaji baada ya makubaliano ya Israel na Hamas ya kustisha mapigano kwa kipindi cha masaa matano kutekelezwa kwa vitendo.

Kauli za wakazi wa Ukanda wa Gaza

Israel Angriffe auf Gaza 16.07.2014

Athari za makombora ya Israel katika Ukanda wa Gaza

Zakaria Ahmed, mwenye umri wa miaka 35, alikuwa miongoni mwa mamia ya watu walikuwa wakijipatia mahitataji hayo muhimu na amenulukiwa na shirika la habari la Uingereza Reuters akisema" Tupa hapa kuchukua mishahara yaetu. Ahsante Mungu kwa utulivu. Tunamatumani Misri itafanikisha hatua ya kweli ya kusitishwa vita, na tuna matumaini mauwaji yatasimamishwa na njia za kuingia katika ukanda wa Gaza zitafunguliwa"

Mkazi mwingine Mohammed Hamdani alionesha wasiwasi wake."Hatua hii ya kuweka silaha chini sio ya kuiaminika. Hawa wanaweza kuwashambulia watu tena .

Hatua hiyo inafanyika saa moja baada ya jeshi la Israel kusema limewazuwia wanamgambo wenye silaha kuingia katika eneo lao ambao walikuwa wakijipenyeza kutoka Gaza.

Jeshi hilo la Israel lilisema kwa kutumia ya andaki kiasi ya wanamgambo 12 wa Kipalestina walipojaribu kuingia Israel kupuitia kwenye handaki wakitokea Gaza Mmoja miongoni mwao aliuwawa baada ya kombora la angani la Israel kuwashambulia.

Kusimamishwa kwa mapigano hayo yaliyodumu kwa siku 10, kunatokana na ombi la Umoja wa Mataifa la kutaka kuruhusu misaada ya kiutu iwafikiwa wakazi wa Ukanda wa Gaza, eneo ambalo linadhibitiwa na kundi la Hamas, ambalo pia linatazamwa na Israel kama kundi la kigaidi.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR/AFP
Mharir:Mohammed Abdul-rahman

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com