Mapigano yaendelea Kongo | Matukio ya Afrika | DW | 29.10.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mapigano yaendelea Kongo

Mapigano mapya yamezuka jana Jumamosi (26.10.2013) kati ya majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi katika siku ya pili ya machafuko ambayo yamesababisha miito ya utulivu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa .

A government soldier holds a position in the eastern Congolese town of Rumangabo, July 26, 2012. Congolese M23 rebels and government forces traded heavy weapons fire around two eastern villages on Thursday in another round of fighting that has forced thousands of civilians to flee towards the provincial capital Goma. REUTERS/James Akena (DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO - Tags: CIVIL UNREST POLITICS CONFLICT)

Mapigano yaongezeka Congo

Mapigano ya hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yamezuka siku ya Ijumaa, chini ya wiki moja baada ya serikali mjini Kinshasa na waasi wa kundi la M23 kutangaza kuwa mazungumzo ya amani mjini Kampala yamevunjika.

Jeshi la serikali jioni ya Jumamosi lilisema kuwa limeukamata mji wa Kibumba , mji ulioko kilometa 25 kaskazini ya eneo mji wa mashariki mwa nchi hiyo wa Goma ambao unatoa njia kuelekea katika eneo la waasi upande wa kaskazini.

Government troops ride on a vehicle towards the frontline where they are fighting against M23 rebels outside the eastern Congolese city of Goma, July 25, 2012. Congolese rebels and government forces traded heavy weapons fire around two eastern villages on Friday, forcing thousands of civilians to flee towards the provincial capital days ahead of a regional summit due to tackle the rebellion. REUTERS/James Akena (DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO - Tags: CIVIL UNREST POLITICS CONFLICT)

Wanajeshi wa serikali Congo

"Kibumba uko chini ya udhibiti wa jeshi la serikali FARDC kuanzia leo," afisa mwandamizi wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP mjini Goma. Waasi hawakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tamko hilo.

Upande mwingine wa mapigano umeanza ghasia siku ya Jumamosi wakati jeshi liliposhambulia maeneo ya kundi la M23 katika jimbo la Mabenga, kiasi ya kilometa 80 kaskazini mwa goma na karibu na mpaka na Uganda.

Jeshi "limeanzisha mashambulizi katika barabara ya Mabenga kuelekea Kahunga. Linatumia wanajeshi, vifaru na makombora", afisa mwingine wa jeshi amesema, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.

Waasi wamethibitisha kuwa mapigano yamesambaa hadi katika eneo la kaskazini.

Mapigano yasambaa

"Mapigano yanaongezeka katika maeneo yote," kiongozi wa kisiasa wa M23 Bertrand Bisimwa amesema katika tovuti ya kundi hilo.

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika mzozo huo, Mary Robinson na Martin Kobler, wametoa taarifa wakielezea wasi wasi wao mkubwa kuhusiana na mapigano hayo mapya.

UN secretary general Ban Ki-Moon (L) signs a guestbook next to Congolese Senate president Leon Kengo Wa Dondo (2nd L) in the Parliament in Kinshasa on May 22, 2013. Ban Ki-moon wraps up a visit to Mozambique and arrives in Kinshasa on a key leg of his Africa trip centred on restoring peace in eastern Democratic Republic of Congo where a flareup in fighting over the past days has left 19 dead. AFP PHOTO/JUNIOR D.KANNAH (Photo credit should read Junior D. Kannah/AFP/Getty Images)

Katibu mkuu wa UM Ban Ki Moon

"Tunatoa wito kwa pande zote kuonyesha hali ya uvumilivu na kuanza tena majadiliano mjini Kampala," wamesema. Marekani imesema kuwa imesitushwa na ripoti za kuongezeka kwa mapigano, licha ya miito ya kimataifa kwa pande hizo kuonesha hali ya kuvumiliana.

"Tunawasi wasi mkubwa juu ya ripoti za mapigano ya mpakani, " katika jimbo la Kivu ya kaskazini, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Jen Psaki amesema katika taarifa, akizitaka pande zinazopigana, "kuacha vitendo vitakavyozidisha hali hiyo".

Taarifa ya Psaki imezitaka pande hizo kurejea katika majadiliano, " ili kuondoa vikwazo vilivyobaki kuelekea kutiwa saini kwa makubaliano ya mwisho, na ya msingi, ambayo yataleta usitishaji wa kudumu wa mapigano na kuwawajibisha wake ambao wamefanya uhalifu mkubwa".

Jumuiya ya kimataifa yaonya

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton pia ametoa wito, "kwa wahusika wote katika eneo hilo kuzuwia kuongezeka zaidi kwa hali hiyo na kuufanya mzozo huo wa kimataifa".

Athari zilizoripotiwa ndani ya mpaka wa Rwanda kutokana na matukio ya hivi karibuni yanapaswa kufanyiwa uchunguzi kwa pamoja," amesema Ashton.

European Union High Representative for Foreign and Security Policy Catherine Ashton speaks to journalists prior to a meeting of Ministers for Foreign Affairs in the Palace of the Grand Dukes of Lithuania in Vilnius on September 6, 2013. AFP PHOTO / TOMAS LUKSYS (Photo credit should read TOMAS LUKSYS/AFP/Getty Images)

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya ,Catherine Ashton

Waasi wanadai kuwa jeshi la serikali lilishambulia maeneo yao mapema siku ya Ijumaa, lakini jeshi la serikali linasisitiza kuwa lilishambuliwa kwanza, madai ambayo yanaungwa mkono na duru kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO.

Wakati huo huo jeshi la serikali ya Kongo limesema limepata mafanikio makubwa dhidi ya waasi wa M23 katika siku ya pili ya mapigano makali jana Jumamosi na kuitaka nchi jirani ya Rwanda kusaidia kuwanyang'anya silaha waasi.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Idd Ssessanga