Mapigano mashariki mwa Kongo | Matukio ya Afrika | DW | 19.11.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mapigano mashariki mwa Kongo

Watu wanaendelea kukimbilia katika makambi ya wakimbizi huko Goma baada ya mapigano yaliyoanza kushuhudiwa tangu jana (18.11.2012) .

Wananchi wakimbilia kwenye kambi ya wakimbizi Goma

Wananchi wakimbilia kwenye kambi ya wakimbizi Goma

Mapambano hayo yalipamba moto jana umbali wa kilomita mbili kaskazini mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Goma, baina ya jeshi la serikali na waasi wa M23.


Majeshi ya serikali pamoja na yale ya Umoja wa mataifa Monusco,yalijaribu kukabiliana na waasi hao bila ya mafanikio.Hata hivyo ghasia hizo zilionekana kutulia baada ya kamanda wa jeshi la Umoja wa mataifa kujadiliana na waasi wa M23.

John Kanyunyu na maelezo zaidi kutoka Beni Kivu ya kaskazini, mashariki mwa DRC.

(Kusikiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi. John Kanyunyu

Mhariri: Yusuf Saumu

Sauti na Vidio Kuhusu Mada