Mapigano mapya yatokea Cote d′Ivoire | Matukio ya Afrika | DW | 24.02.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Mapigano mapya yatokea Cote d'Ivoire

Kiasi ya watu 15 wameuawa katika mapigano mapya yaliyotokea Cote d'Ivoire pale wanajeshi wanaomuunga mkono Laurent Gbagbo walipolivamia eneo ambalo ni ngome ya mpinzani wake mkuu Alassane Ouatarra.

default

Laurent Gbagbo wa Cote d'Ivoire

 Siku moja kabla, wafuasi hao wa Ouatarra walifanikiwa kuwafurusha wanajeshi wa hasimu wake. Ghasia hizo zinatokea wakati ambapo juhudi za kuutanzua mzozo huo kidiplomasia zinaendelea. Mapema wiki hii jopo maalum la marais liliizuru Abidjan na wakakutana na washirika wakuu wa kisiasa wa Cote d'Ivoire. Mzozo huo wa kisiasa umesababishwa na mvutano kati ya Alassane Ouatarra na mpinzani wake mkuu Laurent Gbagbo wanaodai kuwa washindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Novemba mwaka uliopita.

Elfenbeinküste Thabo Mbeki Besuch

Alassane Ouatarra akiwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini,Thabo Mbeki

DW inapendekeza

 • Tarehe 24.02.2011
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10OjE
 • Tarehe 24.02.2011
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10OjE