1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Nyakati mbaya kwa demokrasia nchini DRC

20 Desemba 2018

Vurugu za kabla ya uchaguzi, hofu ya wizi wa kura DRC na kitendo cha kupangwa tarehe ya uchaguzi kufanyika siku mbili kabla ya Krismasi sio bahati mbaya, mkuu wa idhaa ya kifaransa DW anasema.

https://p.dw.com/p/3AQaD
Congolese presidential contender Etienne Tshisekedi
Picha: DW/S. Mwanamilongo

Mtu anaweza kusamehewa kwa kufikiria kwamba uamuzi wa kuandaa uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo tarehe 23 si bahati mbaya. Ni wakati ambapo nusu ya idadi ya watu nchini humo hawatafikiria suala jingine ila Krismasi. Vile vile ni wakati mzuri wa uchaguzi ambao hautavutia ukosoaji mkubwa wa kimataifa kuhusiana na visa vya wizi wa kura, matatizo katika usimamizi wa uchaguzi wenyewe au vitendo vya ukandamizaji.

Uchaguzi huo umegubikwa na ghasia ambazo zimesababisha watu kadhaa kuuawa. Wagombeaji wa upinzani wamelalamikia kutishiwa na kunyanyaswa. Lakini miongoni mwa wafuasi wao pia kuna baadhi ya wanasiasa ambao ni  kila kitu  lakini sio wademokrasia, kwa mfano aliyekuwa makamu wa rais na aliyewahi kuwa mkuu wa wanamgambo nchini DRC, Jean Pierre Bemba ambaye Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC ilimkuta na hatia ya kuhonga mashahidi.

DR Kongo Wahlkampf in Kinshasa
Picha: Getty Images/AFP/S. Tounsi

Kimsingi pia, maandalizi ya uchaguzi wenyewe yako katika hali ya machafuko. Katika nchi hiyo iliyo na miundo mbinu kidogo inayofanya kazi, kuna baadhi ya maeneo ambayo hayana vifaa vinavyohitajika kuandaa uchaguzi. Eneo la Mashariki ,mripuko wa ugonjwa wa Ebola bado haujadhibitiwa. Kuna pia makundi yenye silaha ambayo yanawaua raia karibu kila siku, na ambao wanafanya hali kuwa ngumu uchaguzi kufanyika.

Kilichotokea tarehe 13 mwezi huu kimefanya mambo kutokuwa wazi. Siku kumi kabla ya uchaguzi moto uliteketeza ghala lililotumiwa na Tume ya Uchaguzi katika mji mkuu Kinshasa. Ghala hilo lilikuwa na thuluthi mbili ya vifaa vya uchaguzi kwa mji huo,ikiwemo mashine elfu nane miongoni mwa  mashine zaidi ya elfu kumi zilizotarajiwa kutumiwa na wapiga kura wa mji wa Kinshasa.

Demokratische Republik Kongo Wahlmaschine
Picha: Getty Images/AFP/J. Wessels

Kuna uwezekano mkubwa kwamba ikiwa  uchaguzi utafanyika  tarehe 23 mwezi huu, kutashuhudiwa ghasia zaidi. Lakini pengine mpaka pale watu wengi watakapouwawa na kuzuka machafuko makubwa  ndipo ndipo dunia itakapoweza kutambua kinachoendelea kutokana na msimu huu wa mwaka. Hata kukiwepo visa vingi vya wizi wa kura huenda visiwavutie watu katika mataifa mengine.

Mwandishi: Sophia Chinyezi/DW

Mhariri: Saumu Yusuf