1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manchester City bingwa mara tatu

20 Mei 2019

Manchester City wameandika historia nchini humo kwa kuwa timu ya kwanza kabisa kunyakua vikombe vitatu kwa nyumbani. Miamba hao wameshinda taji la Carabao, Ligi Kuu na FA Cup.

https://p.dw.com/p/3ImDO
FA Cup Finale | Manchester City v Watford | Manchester City Mesiter
Picha: picture-alliance/empics/N. French

Manchester United walishinda vikombe vitatu msimu wa mwaka 1998/1999 lakini vikombe viwili vilikuwa vya nyumbani, Ligi Kuu na FA Cup ila taji la tatu likawa Ligi ya Vilabu bingwa.

Lakini licha ya kushinda mataji yote hayo, kocha wa City Pep Guardiola anasema kikosi chake hakitahesabika kama mojawapo ya kikosi bora katika historia kama hawatoshinda Champions League.

Premier League: Brighton & Hove Albion v Manchester City
Kocha wa Man City Pep GuardiolaPicha: Getty Images/M. Hewitt

"Nimeshasema hapo awali, najua mwishowe tutatathminiwa. Iwapo hatutashinda Champions League haitatosha, hilo najua. Nilikuwa na bahati Barcelona kwasababu nililishinda taji hilo mara mbili katika miaka minne. Vikombe vya nyumbani ni muhimu kuvishinda ila Champions League ni muhimu zaidi lakini unahitaji kufanya kazi ya ziada kwasababu timu zengine ni nzuri sana," alisema Guardiola.

Manchester City lakini wamepata pigo kwa kuwa nahodha wao Vincent Kompany ametangaza kuwa anaelekea katika klabu ya Anderlecht nchini Ubelgiji kuwa mchezaji na kocha pia.

Kompany ameichezea City kwa kipindi cha miaka kumi na moja.