1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manasseh Rukungu

7 Oktoba 2003
https://p.dw.com/p/CHM3

Gazeti mashuhuri kimataifa Die Welt, linapozingatia kule kukubaliwa mapendekezo ya inayojulikana kama Tume ya Herzog ya kuboresha huduma za kijamii hapa nchini, linaandika: Kukubaliwa kwa mapendekezo hayo kunathibitisha jinsi chama cha CDU kilivyoshindwa katika siasa zake binafsi za mageuzi. Mapendekezo hayo hata yamekubaliwa kwa kauli moja na tawi madhubuti la wale wanaounga siasa za ajira katika chama hiki cha waKrist-demokrats akiwemo waziri wa zamani wa ajira Nobert Blüm. Lakini ufafanusi zaidi hakuna. Inaelekea hadi sasa ni chama hiki cha upinzani pekee CDU, ambacho kikiwa chini ya uongozi wa Angela Merkel, kimepata mafunzo kutokana na makosa ya Kansela. Wanachama wa CDU wameanza na majadiliano wakati unaofaa pindi kukiokoa chama kutokana na hali isiyo ya kijadi. Nalo gazeti mashuhuiri la shuguli za biashara la mji wa magharibi wa Düsseldorf, Handelsblatt, kuhusu mada hii linahariri: Baada ya uongozi wa chama cha CDU kuyakubali mapendekezo hayo ya Tume ya Herzog, alao kwa kura mbili tu, sasa kuna matumaini kwamba, enzi ya kutokuwa na mwelekeo wa kiuchumi ya zamani ya Ludwig Erhard, imehitimika. Kiongozi wa kundi la chama cha CDU bungeni, Friedrich Merz, alieleza waziwazi kuhusu mada hii kwamba, sasa umefikiwa mwanzo wa mwisho wa siasa za huduma za kijamii katika chama hiki. Lakini si yeye wa kutolewa shukurani katika pindukio hili, bali ni mwenyekiti wa chama Angela Merkel.

Gazeti mojawapo mashuhuri la kusini mwa Ujeqrumani, Frankfurter Rundschau, linajishugulisha na mada ya nje kwa kutupia jicho matokeo ya uchaguzi katika Jamhuri inayotaka kujitenga ya Chechnia kwa kuandika: Serikali ya Moscow inaridhika na matokeo ya kuchaguliwa kiongozi mpya wa jamhuri hiyo Ahmad Kadyrow, lakihni isisahauliwe kwamba, matokeo hayo yanatokana na kushiriki raia wengi wa asili ya Russia, ndio maana wadadisi wengi wa kimataifa hawaoni chochote cha kulaumiwa au cha kukosolewa. Taarifa hii njema imetangazwa kwa fahari na vyombo vyote vya habari vya kiRussia vilivyoko kaskasini mwa Jamhuri hiyo ya Kaukasus. Hata hivyo hapa linazuka swali kama haya ni matokeo ya uchaguzi ambayo bunge la Moscow Duma linaweza kujivunia kwa kweli? Naam, mtu anaweza kujibu ni matokeo ya kuwaridhisha wabunge hasa kwa sababu mgombea wa wadhifa huo aliteuliwa na serikali ya Moscow binafsi.

Kinyume cha hayo gazeti mojawapo mashuhuri la hapa mjini Bonn, Bonner General Anzeiger, kuhusu kuteuliwa Bw.Kadyrow na serikali ya Moscow linasema. Hakuna mtu anayeweza kushikilia kwamba, uchaguzi wa rais katika Chechnia umefanyika chini ya misingi ya demokrasia. Kwani baada ya rais wa Russia Wladimir Putzi kuwaondolea mbali kijanja wagombea wengine, wapigaji kura hawakuwa na mwingine wa kuchagua isipokuwa Ahmad Kadyrow pekee. Kuna sababu zake: Rais Putin anataka kuona amani ikihifadhiwa tena huko Chechnia na ujenzi mpya Jamhuri hiyo ukipigwa jeki, ijapokuwa jamhuri hii inayotaka kujitenga iko nje ya shirikisho la Russia na haina matumaini makubwa ya kuweza kujitawala wakati unao.

Gazeti lingine mashuhuri la kusini mwa Ujerumani Frankfurter Allgemeine Zeitung, linakamilisha mada hii kwa kuandika: Kile Wachechnia wanataka kuona, ni kukomeshwa mauaji na kuhifadhiwa tena usalama nchini mwao. Hawataki tena kuona kwamba, usemi kamili uko mikononi mwa rais wa zamani Maschadow, ambaye kwa siasa zake kali za kiislamu wanamlaumu kwa sababu ya kuwazushia matatizo machungu tangu miaka mingi. Ijapokuwa hayo hata hawampendelei sana halikadhalika rais mpya Kadyrow, kwa sababu wanahisi hatawaletea kile wanachotaka. Mapigano bado yanaendelezwa kutoka kila upande kwa mikakati ya kigaidi. Hata baadhi ya wafuasi wa rais mpya wanaloweshwa mikono yao na damu ndio maana wameshatangaziwa hatua za kisasi. Hali hii inaonyesha kwamba, swala la Chechnia litakuwa gumu kutatulika, hasa mtu akiona jinsi serikali ya Kremlin inavyopuuza masilahi ya raia wa Jamhuri hiyo.