1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man Utd wawazidi ujanja Liverpool

25 Januari 2021

Hapo Jumapili kulikuwa na mechi ya raundi ya nne ya kombe la FA iliyowapatanisha Manchester United na Liverpool huko England.

https://p.dw.com/p/3oNtw
Fußball Edison Cavani Manchester United
Picha: Martin Rickett/PA Wire/picture alliance

United waliwazidi kete Liverpool magoli 3-2 uwanjani Old Trafford. Sasa baada ya ushindi huo, kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solksjaer anasema timu yake inazidi kuimarika.

"Ni vizuri sana kushinda mechi dhidi ya mabingwa wa ligi wa mwaka jana, timu nzuri sana na katika miaka michache iliyopita tulipokuwa tukicheza na timu tofauti tumepata matokeo mazuri. Tumepata njia ambayo tunaiamini, wachezaji wanaiamini na tunazidi kuimarika.

Tumeonyesha mara kadhaa msimu huu uwezo wa kutoka nyuma baada ya kufungwa na kushinda mechi, hilo hata mimi mwenyewe nahisi," alisema Solksjaer.

Lakini kocha wa Liverpool Jurgen Klopp hana wasiwasi licha ya timu yake kuonyesha msururu wa matokeo yasiyoridhisha mwezi huu wa Januari.

"Lakini haustahili kuwa na wasiwasi na sisi, tuko kama kikundi, tuko pamoja na tunajua kama nina tatizo basi tuna tatizo na hilo ndilo tatizo letu kwasasa na ni lazima tulisuluhishe kwa pamoja na hivyo ndiyo tutkavyofanya. Hakuna anayefikiria yale mazuri yaliyofanyika miaka kadhaa iliyopita, hakuna, tuko katika wakati wa sasa na tutajaribu kushinda mechi tena na hivyo ndivyo ilivyo," alisema Klopp.