1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man United washindwa kuivunja ngome ya Liverpool

20 Januari 2020

Rekodi ya Liverpool ya kutofungwa msimu huu bado ingalipo baada ya kuwalaza Manchester United hapo Jumapili uwanjani Anfield kwa magoli mawili kwa bila, Virgil van Dyke na Mohammed Salah wakiwa wafungaji wa mabao hayo.

https://p.dw.com/p/3WU43
Fussball Champions League l Red Bull Salzburg vs Liverpool l Tor 0:1 Jubel
Picha: Reuters/J. Sibley

Rekodi ya Liverpool ya kutofungwa msimu huu bado ingalipo baada ya kuwalaza Manchester United hapo Jumapili uwanjani Anfield kwa magoli mawili kwa bila, Virgil van Dyke na Mohammed Salah wakiwa wafungaji wa mabao hayo.

Kwa ushindi huo Liverpool wameongeza tofauti ya pointi zao na Manchester City ambayo ndiyo timu iliyo kwenye nafasi ya pili na kufikia pointi kumi na sita kwa sasa huku wakiwa na mechi moja ambayo hawajacheza.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alikuwa na haya ya kusema baada ya mechi hiyo.

"Tunaamini kwamba matokeo yanaashiria jinsi tulivyocheza. Ukiangalia jinsi tulivyocheza dakika tisini au zaidi kwa kweli tulistahili kushinda. Na hivyo ndivyo tunavyotaka," alisema Klopp.

United walikosa nafasi za wazi katika mechi hiyo na kocha wao Ole Gunnar Solksjaer amesema huenda wakatafuta washambuliaji katika dirisha hili la uhamisho.

"Unapowakosa kikosini mwako wachezaji kama Scott McTominay, Paul Pogba na Marcus Rashford bila shaka mapungufu yataonekana tu. Kwa hiyo tutasajili wachezaji labda kwa mkopo watakaotusaidia kwa muda mfupi hadi msimu wa majira ya joto," alisema Solksjaer.