Man City yaurefusha mkataba wa Pellegrini | Michezo | DW | 07.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Man City yaurefusha mkataba wa Pellegrini

Manchester City imempa kocha Manuel Pellegrini kura kubwa ya kuwa na imani nae katika mkesha wa msimu mpya wa kandanda, kwa kuurefusha mkataba wake kwa miaka miwili zaidi.

Manchester City imempa kocha Manuel Pellegrini kura kubwa ya kuwa na imani nae katika mkesha wa msimu mpya wa kandanda, kwa kuurefusha mkataba wake kwa miaka miwili zaidi.

Hivyo kocha huyo wa Chile mwenye umri wa miaka 61, atasalia katika klabu hiyo hadi Juni 2017pamoja na makocha wasaidizi Ruben Cousillas, Xabier Mancisidor na Jose Cabello.

Wakaosoaji wameashiria kuwa Pellegrini atapigwa kalamu ikiwa City haitaipokonya Chelsea taji la ligi kuu ya Premier lakini kocha huyo, aliyejiunga na City mwaka wa 2013 anaamini watakuwa na msimu mzuri zaidi.

City wataanza kampeni yao ugenini dhidi ya West Bromwich Albion Jumatatu na watakabana koo na Chelsea katika mchuano wao wa kwanza wa nyumbani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Iddi Sessanga