1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man City yatawazwa ubingwa wa PL

12 Mei 2021

Klabu ya Manchester City inayoshiriki ligi kuu ya England imetawazwa ubingwa wa ligi hiyo ya Premier League, ikiwa ni mara ya tatu katika misimu minne.

https://p.dw.com/p/3tGwY
Champions League Halbfinale - Manchester City v Paris St Germain Tor: (2 : 0)
Picha: Phil Noble/REUTERS

Klabu ya Manchester City inayoshiriki ligi kuu ya England imetawazwa ubingwa wa ligi hiyo ya PL, baada ya Manchester United kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Leicester.

Manchester City inatawazwa mabingwa kwa mara ya tatu katika kipindi cha misimu minne, ikiwa na pointi kumi mbele ya United na inachukua ubingwa ikiwa bado na michezo mitatu mkononi.

Kocha wa kikosi hicho Pep Guardiola amesema haukuwa msimu mwepesi na wataukumbuka wakati wote, kutokana na vizuizi na changamoto walizokabiliana nazo hususan kutokana na janga la virusi vya corona.