1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man City waweka rekodi ya mataji ya Carabao

26 Aprili 2021

Manchester City Jumapili waliweka rekodi kwa kushinda taji la Carabao kwa msimu wa nne mfululizo katika fainali dhidi ya Tottenham Hotspur iliyochezwa uwanjani Wembley.

https://p.dw.com/p/3sbBA
Champions League I Borussia Dortmund v Manchester City
Picha: Wolfgang Rattay/REUTERS

Goli la pekee lilifungwa na Aymeric Laporte na wachambuzi wa kandanda wanasema huenda mambo yangekuwa tofauti iwapo Spurs hawangemfuta kazi Jose Mourinho, siku chache kabla ya fainali hiyo kwani kocha wa muda wa Spurs Ryan Mason alionekana kutokuwa na mbinu za kuikabili City.

Mashabiki, ingawa si wote, waliruhusiwa kuingia na kuitazama mechi hiyo na ni jambo ambalo lilimfurahisha Guardiola.

"Uwanja haukujaa ila waliwakilisha mashabiki wote kwa hiyo kusherehekea nao ushindi huu ni jambo zuri. Walitushabikia kwa dhati, kwa hiyo ni jambo zuri bila shaka. kwa kawaida tunashinda kwasababu yao," alisema Guardiola.

Kocha wa muda wa Spurs Ryan Mason alikuwa na haya ya kusema baada ya mpambano huo.

"Ni vigumu kukubali, ni vigumu kukubali ukiwa na wachezaji kama hawa na hata kwa mtu yeyote anayehusika na klabu hiki lakini tunastahili kusonga mbele," alisema Mason.