Mamluki Simon Mann ahukumiwa miaka 34 jela | Habari za Ulimwengu | DW | 08.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mamluki Simon Mann ahukumiwa miaka 34 jela

-

MALABO

Mamluki wa kiingereza Simon Mann amehukumiwa kifungo cha miaka 34 jela na mahakama ya Guinea Equator baada ya kukutwa na hatia juu ya mashatka ya kuhusika na njama zilizoshindwa kufanikiwa za kuipindua serikali ya nchi hiyo mwaka 2004 njama ambayo alisema inamhusisha pia mwanawe waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Magraret Thacher,Mark Thatcher.

Mawakili wa Simon wanaweza kukataa rufaa kwenye mahakama kuu ya Guinea Equator au kuomba msamaha moja kwa moja kwa rais Teodoro Obiang Nguema dhidi ya hukumu hiyo iliyotolewa jana na jaji Carlos Mangue chini ya ulinzi mkalai mjini Malabo.

Simon alitoa ushahidi na kukiri makosa akisema alitumiwa na vigogo wa kibishara wa kimataifa wakiwemo millionea Eli Cali na Mark Tharcher ambao walitaka kujaribu kumuingiza madarakani mshirika wao kiongozi wa upinzani anaishi uhamishoni Severo Moto.

Mann alikamatwa miaka minne iliyopita na maafisa wa Zimbabwe pamoja na mamluki wenzake 70 wakiwa njiani kuelekea Guienea Equator kutekeleza jaribio la mapinduzi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com