MALUKU INDONESIA:Volcano yasababisha maelfu kukimbia makazi yao | Habari za Ulimwengu | DW | 11.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MALUKU INDONESIA:Volcano yasababisha maelfu kukimbia makazi yao

Maelfu ya watu wamekimbia kwenye vijiji vya mkoa wa kaskazini wa Maluku nchini Indonesia kufuatia miripuko kadhaa ya Volcano na kuanza kutoa majivu ya moto na moshi.

Mlima wa Gamkonora uliripuka mara tatu kwa kishindo kikubwa na kusabababisha wakaazi 8000 kutoka vijiji tisa vilivyoko kwenye eneo la mlima huo kuondoka.Bado juhudi za kuwaondoa watu wengine kiasi cha 5000 zinafanyika kwenye eneo hilo.

Hadi sasa hakuna mtu aliyejeruhiwa kufuatia kuripuka kwa volcano hiyo.Mlima Gamkonora umeshawahi kuripuka mwaka 1997 na hakuna mtu aliyeuwawa kwenye tukio hilo lakini maelfu ya watu walilazimika kukimbia eneo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com