Maktaba zinazoongoza kwa ubora duniani
Maktaba zimekuwepo kwa miaka zaidi ya 4000. Zinaweza kuwa kama kumbi za dansi lakini bila kujali namna gani zinaonekana, Maktaba ni maeneo mazuri ya kusherehekea Siku ya Kitabu Duniani kwa mwaka huu, Aprili 23.
Kutoka kuporomoka hadi hali bora
Maktaba ya mke wa Bintimfalme Anna Amalia huko Weimar ilipata jina lake la sasa mwaka 1991. Awali iliitwa "maktaba ya bintimfalme" kwa miaka 300. Jengo lenye ukumbi maarufu wa juu liliharibiwa kwa moto, lakini lilifunguliwa tena Oktoba 24, 2007, takribani miaka 10 iliyopita.
Uwanja wa mpira au Maktaba?
Usihofu kama huna kitambulisho cha mwanafunzi, maktaba ya Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Delft nchini Uholanzi ni ya kutembelea hata bila hicho. Jengo la vioo la juu kwenye nyasi ni la kushangaza sana, na urefu wa jengo la mita 42 mfano wa koni katikati linaficha ghorofa nne zilizosheheni vitabu.
Mbao za Mninga
Gazeti la Uingereza "The Daily Telegraph" lilijumuisha Maktaba ya Joanina huko Coimbra, Ureno katika orodha ya maktaba ya ajabu sana duniani mwaka 2013. Inaitwa jina la mfalme wa Kireno, John V, ambaye aliamuru ujenzi wake. Vitabu vyote vya vitabu vitengenezwa kwa mbao za mninga na mahali hapo sasa ni sehemu ya Kitivo cha Sheria.
Dunia ya kale yakutana na ya sasa
Maktaba ya Alexandria nchini Misri ilikuwa maktaba maarufu zaidi ulimwenguni kabla ya kuharibiwa kwa moto karibu miaka 2,000 iliyopita. Inasemekana kuwa imejumuisha ujuzi wote wa ulimwengu katika mistari 490,000 ya karatasi za mafunjo. Maktaba mpya ya Alexandria, ambayo inaendeleza jadi, ilifunguliwa mwaka 2002. Gharama yake ya mwisho? Zaidi ya dola milioni 220, sawa na yuro milioni 187 .
Miongoni mwa miundo ya zamani
Baadhi ya vielelezo vinavyomilikiwa na maktaba ya Abbey Saint Gall huko St. Gallen, Uswisi vina umri wa miaka zaidi ya 1,300, na wageni wanaweza kuona mchoro wa jengo la watawa, mchoro wa zamani wa jengo barani Ulaya, au mabaki ya miili ya binadamu wa Misri. Ukumbi wa juu wa vitabu upo katika turathi ya UNESCO tangu mwaka 1983.
Iliokolewa na rais
Tembelea maktaba ya bunge wakati wowote unapokwenda Washington, D.C. Maktaba hii ilianzishwa mwaka 1800 lakini iliteketezwa na Waingereza miaka 14 baadae. Thomas Jefferson, rais wa tatu wa Marekani, aliuza karibu vitabu 6500 kutoka maktaba yake binafsi ili kufadhili gharama ya dola 24,000 za ukarabati. Chumba kikuu cha kusomea hapo juu pichani kilijengwa katika mtindo wa karne ya 19.
Wazo la mwaloni
Ghorofa mbili "chumba cha kale" katika maktaba ya chuo cha zamani cha Trinity mjini Dublin ina urefu wa mita 64 na upana wa mita 12. Lakini nafasi hiyo haikuwa ya kuvutia kama ilivyo sasa. Dari yake iliondolewa 1858 na kubadilishwa na paa la mwaloni.
Kila kitu ni kikubwa China
Ikiwa na nyaraka zaidi ya milioni 30 za vitabu na taarifa nyingine, maktaba ya taifa ya China ni mojawapo ya maktaba 7 kubwa duniani. Ilijengwa kama "makatba kuu" mwaka 1809 na baadae kupewa jina la "maktaba ya Beijing" mwaka 1928 baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuanzishwa. Jina lake la sasa lilipitishwa na serikali mwaka 1998.