Magwiji wateremka dimbani Wimbledon | Michezo | DW | 08.07.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Magwiji wateremka dimbani Wimbledon

Wachezaji nyota Serena Williams, chipukizi Coco Gauff na majina makubwa ya tennis kwa wanaume Roger Federer, Rafael Nadal na Novak Djokovic wanateremka dimbani Jumatatu.

Nyota hao wanashiriki wiki ya pili ya mashindano ya Wimbledon huko Uingereza.

Mechi zote kumi na sita zimepangiwa kuchezwa Jumatatu baada ya mapumziko Jumapili.

Gauff atakuwa anapambana na mchezaji nambari moja wa zamani Simona Halep huku Serena Williams akitafuta kufuzu raundi inayofuata kwa kuchuana na Carla Suarez Navarro.

Djokovic, Nadal na Federer wote wanacheza na wachezaji ambao hawajawahi kushiriki Wimbledon.