1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBrazil

Mafuriko, maporomoko yaua watu 75 nchini Brazil

6 Mei 2024

Mafuriko makubwa katika jimbo la kusini mwa Brazil la Rio Grande do Sul yamesababisha vifo vya watu 75 na wengine 103 hawajulikani walipo katika kipindi cha siku saba zilizopita.

https://p.dw.com/p/4fXbN
Canoas nchini Brazil 2024 | Eneo la mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha
Mafuriko katika eneo la Canoas jimbo la Rio Grande do Sul nchini BrazilPicha: Amanda Perobelli/REUTERS

Watu wasiopungua 155 wamejeruhiwa huku mafuriko hayo yakiwalazimisha zaidi ya watu 88,000 kuyakimbia makazi yao.

Mamlaka zinasema kwamba watu wengine 16,000 wamepewa hifadhi kwenye majengo ya shule, kumbi za mazoezi na makaazi ya muda.

Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa yamesababisha maporomoko ya udongo, kusomba barabara na kuvunja madaraja ya jimbo hilo.

Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil amelitembelea jimbo hilo kwa mara ya pili siku ya Jumapili akiwa ameongozana na mawaziri kukagua uharibifu uliotokea.