Sheria na HakiUlaya
Maelfu wajitokeza kumzika Navalny aliefariki gerezani
2 Machi 2024Matangazo
Waombolezaji hao walikabiliwa na maia ya polisi wakati wakielekea katika kanisa ambako msiba wa Navalny ulifanyika, na katika makaburi alikozikwa.
Waombolezaji hao ambao walipanga foleni kwa muda mrefu ili kuweka mauwa katika jeneza la kiongozi huyo mashuhuri wa upinzani, walipaza sauti wakimshutumu rais Vladmir Putin.
Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la OVD-Info, linalofuatilia ukamataji wa kisiasa, takriban wati 91 walikamatwa kote nchini Urusi katika matukio ya kumuenzi Navalny.
Soma pia:Navalny atarajiwa kuzikwa kusini mwa jiji la Moscow
Mamlaka nchini Urusi bado haijaweka wazi sababu ya kifo cha mwanasiasa huyo hadi sasa, ingawa watu wake wanataja kuwa nyaraka ambazo wameziona zinaonesha kifo hicho ni cha asili.