Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Ripota wa Aljazeera auawa katika uvamizi wa Israel Ukingo wa Magharibi/ Rais wa Tanzania atarajiwa kukamilisha ziara yake ya kikazi Uganda/ Ukraine yasitisha usafirishaji gesi kupitia Luhansk/ Kongo: Jaji Dieudonné Kaluba Dibwa amefutwa kazi/ Mahojiano kuhusu mchakato wa uteuzi wa jaji mkuu nchini Kongo na ikiwa hatua hii itachangia kutuliza uhasama baina ya chama tawala na upinzani
Kadiri bei ya mafuta inavyopanda, mtindo wa kuendesha gari kwa kasi unaweza kukugharimu sana pesa. Hapa kuna vidokezo vya kuhifadhi mafuta.
Umoja wa Ulaya walaani hatua ya Urusi kusitisha usambazaji wa gesi kwa mataifa ya Ulaya // Mkuu wa Umoja wa Mataifa awasili mjini Kyiv kwa mazungumzo na uongozi wa Ukraine // Na Baraza la Seneti Nigeria lapitisha muswada unaoharamisha malipo ya kikomboleo
Waandamanaji nchini Ujerumani wanaishinikiza serikali yao kukubali kutonunua mafuta na gesi kutioka Urusi, wanasema fedha wanazozipata zinafadhili vita,mauaji na uteswaji wa raia Ukraine
Rais Putin atishia kusitisha mikataba ya kusambaza gesi ya Urusi barani Ulaya // Umoja wa Mataifa waidhinisha ujumbe mpya wa Umoja wa Afrika nchini Somalia // Na wafadhili wa kimataifa waahidi dola bilioni 2.44 katika msaada kwa Afghanistan
Vikosi vya Urusi vyashambulia kituo kikubwa cha kijeshi cha Ukraine karibu na mpaka na Poland. Viongozi wa Uturuki na Ugiriki kukutana leo juu ya vita ya Ukraine. Na kampuni ya gesi ya Urusi yasema itaendelea kusafirisha nishati hiyo kulingana na mkataba licha ya vita inayoendelea.
Juhudi za kuwaondoa maelfu ya watu waliokwama Ukraine/ Tanzania ambayo ilishagundua gesi asilia, inaweza kuchukua nafasi hii na kuuza gesi yake asilia kimataifa?/ Miaka 4 ya makubaliano kati ya Kenyatta na Raila/ Kenya: Miaka minne sasa tangu salamu hizo za kheri / Mashambulizi ya ndege yamesababisha vifo vya raia 304 katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia tangu mwezi Novemba
Ikulu ya Urusi imesema kwamba hakuna mipango kamili ya kufanyika mkutano wa kilele juu ya Ukraine kati ya Putin na Biden/ Mawaziri wa mambo ya nje wa EU wakataa kuiwekea vikwazo Urusi/ Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania kimetoa ripoti ya mfano ya utafiti wake kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia wilaya ya Kinondoni/ Qatar: Mkutano wa kilele kuhusu gesi
Rais wa Marekani Joe Biden aonya kuhusu mradi wa bomb ala gesi la Nord Stream 2. Rais wa Urusi Vladimir Putin asema nchi yake haihusiki na wakandarasi wa kibinafsi wa kijeshi wa Urusi nchini Mali. Na mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kuendelea leo mjini Vienna, Austria.
Human Rights Watch: Haki bado haijapatikana tangu kufanyika vurugu kwenye uchaguzi mkuu wa visiwani Zanzibar/ Siku ya Ukimwi duniani yaadhimishwa/ Tamko la WHO kuhusu kuzuka kwa aina mpya ya kirusi cha corona/ Oparesheni ya pamoja kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo/ Ujerumani imeahirisha kutoa idhini kwa kampuni inayoendesha mradi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Kenya, Henriette Gieger ameonesha wasiwasi wake kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini Kenya, huku visa vya ukosefu wa usalama vikishuhudiwa kwenye kampeni. Huku tahadhari kuhusiana na jinsi mabadiliko ya tabia nchi yatakavyouathiri ulimwengu katika miongo ijayo zikizidi, makampuni makubwa makubwa yameanza kudhamiria kupunguza utoaji wa gesi chafu hewani.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dokta Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa serikali yake imejifunza makosa ya mataifa mengine juu ya dhana ya laana ya rasilimali katika kipindi ambacho serikali yake inaendelea na utafiti wa mafuta na gesi asilia ndani ya Bahari ya Hindi. Dotto Bulendu. amefanya mahojiano maalumu na Dr. Mwinyi.
Rais wa Zanzibar Dokta Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa serikali yake imejifunza makosa ya mataifa mengine juu ya dhana ya laana ya rasilimali katika kipindi ambacho serikali yake inaendelea na utafiti wa mafuta na gesi asilia ndani ya Bahari ya Hindi. DW imemtembelea Rais Mwinyi Ikulu ya Mnazi Mmoja huko Zanzibar na kuzungumza naye katika mazungumzo yaliyoendeshwa na mwandishi wetu Dotto Bulendu.
Bei ya mafuta imepanda kote ulimwenguni jambo ambalo limesababisha bei za bidhaa nyengine muhimu kupanda pia na kuongeza gharama za maisha. Bei za gesi na maka ya mawe pia zimepanda na kufikia viwango vipya vya kuvunja rekodi. Josephat Charo analiangazia suala hili katika maoni mbele ya meza ya mduara leo.
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa janga la COVID-19 halijapunguza kasi ya mabadiliko ya tabia nchi ulimwenguni. Kwenye makala hii ya Mtu na Mazingira Saleh Mwanamilongo anaangazia kwa nini viongozi duniani bado hawajapunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa gesi chafu na kufikia malengo ya mkataba wa Paris wa mwaka 2015?
Bei ya mafuta imepanda kote ulimwenguni hali ambayo imesababisha bei za bidhaa nyingine muhimu kupanda na kuongeza gharama za maisha. Bei ya mafuta imeongezeka hadi kufikia zaidi ya dola 80 kwa pipa huku bei za gesi asili na makaa ya mawe zikifikia viwango vipya na kuvunja rekodi katika wiki chache zilizopita. Josephat Charo anajadili suala hili katika kipindi cha Maoni mbele ya Meza ya Duara.
Kenya imepuuzilia mbali uamuzi uliotolea na Mahakama ya Haki ya Kimataifa ICJ kuhusu mpaka wake na Somalia kwenye bahari ya Hindi. Rais Uhuru Kenyatta amelaani uamuzi huo akisema kuwa Kenya haitakubali kamwe unyakuzi wa ardhi yake. Kwa upande wake Somalia imepongeza hatua hiyo baada ya Mahakama ya ICJ kuipa kipande kikubwa cha eneo hilo linalozozaniwa na mataifa hayo.
Makala ya Mwangaza wa Ulaya inamulika kukamilika kwa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Urusi hadi Ujerumani licha ya upinzani mkali ulioliandama bomba hilo maarufu kama Nord-Stream 2, hususan kutoka Marekani na Ukraine.
Wataliban hawataongeza muda wa kuhamishwa watu/ Marekani imejikita katika kuondoa vikosi vyake Afghanistan/ Congo- Kivu Kusini: Shughuli za kampuni sita za china za uchimbaji madini zimesimamishwa ili kuhifadhi maslahi ya wakaazi wa vijiji kunakochimbwa dhahabu na pia kurejesha utulivu / Merkel, Zelensky waujadili mradi wa gesi wa Nord Stream 2
Shirika la WFP latoa tahadhari juu ya kutokea kwa janga la kibinadamu nchini Afghanistan, rais Joe Biden amshukuru Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Abu Dhabi, Sheikh Mohammed Bin Zayed al- Nahyan kwa msaada nchini Afghanistan na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ataka ufafanuzi zaidi kuhusu kile kitakachotokea baada ya kumalizika kwa mkataba wa usafirishaji gesi kati yake na Urusi mnamo mwaka 2024