Mabingwa Dortmund waambulia sare | Michezo | DW | 08.10.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mabingwa Dortmund waambulia sare

Mabingwa watetezi Borussia Dortmund waambulia sare na Hannover 96 ,wakati Bayern Munich yazidi kuchanja mbuga. Messi na Ronaldo ngoma droo katika el classico uwanjani Nou Camp mjini Madrid.

GettyImages 153614454 Dortmund's Polish striker Robert Lewandowski (R) celebrates scoring a goal with team mates Dortmund's Polish defender Lukasz Piszczek (C) and Dortmund's striker Marco Reus (L) during the German first division Bundesliga football match Hannover 96 vs Borussia Dortmund in Hannover on October 7, 2012. AFP PHOTO / ODD ANDERSEN (Photo credit should read ODD ANDERSEN/AFP/GettyImages)

Wachezaji wa Borussia Dortmund wakishangilia bao dhidi ya Hannover

Tukianza na ligi ya hapa ujerumani , Bundesliga, mabingwa watetezi Borussia Dortmund walibidi kukubali sare ya bao 1-1 dhidi ya Hannover 96 katika pambano ambalo lilikuwa na hamasa nyingi siku ya Jumapili (07.10.2012), nyumbani kwa Hannover.

Lakini sare hiyo imewagharimu mabingwa hao watetezi baada ya kuwapoteza wachezaji watatu katika mchezo huo wakiwa majeruhi. Yakub Kuba Blaszczykowski , mlinzi Matts Hummels nahodha Sebastian Kiel na mlinzi wa kati Sven Bender walibadilishwa kutokana na maumivu waliyoyapata katika mchezo huo, ambao kama kawaida yao Borussia walionyesha mchezo wa kasi, lakini hatimaye hawakupata matokeo waliyoyahitaji.

GettyImages 153614459 HANNOVER, GERMANY - OCTOBER 07: Jakub Blaszczykowski of Dortmund is seen injured during the Bundesliga match between Hannover 96 and Borussia Dortmund at AWD Arena on October 7, 2012 in Hannover, Germany. (Photo by Joern Pollex/Bongarts/Getty Images)

Jacub Kuba wa Borussia Dortmund akipatiwa matibabu

Kushindwa kwa Borussia kupata points tatu katika mchezo huo kumeiweka Bayern Munich katika nafasi salama ya uongozi wa ligi hiyo baada ya michezo saba ya ligi, ambapo inaongoza kwa points 21, ikiipita Borussia kwa points 9 na iko katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.

Hannover yapigana kiume

Baada ya bao la Robert Lewandowski , kikosi cha kocha Mirko Slomka wa Hannover kilipigana kufa na kupona na alikuwa mshambuliaji aliyeazimwa kutoka Manchester United , Mame Diouf aliyewaliza Dortumnd katika dakika ya 86 kwa bao la kusawazisha baada ya Dortmund kushindwa kuuondoa mpira langoni mwao.

Fußball, Bundesliga, 7. Spieltag, Hannover 96 - Borussia Dortmund am Sonntag (07.10.2012) in der AWD-Arena in Hannover: Der Hannoveraner Spieler Mame Diouf bejubelt seinen Treffer zum 1:1 gegen Borussia Dortmund. Foto: Peter Steffen dpa (Achtung Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine videoähnlichen Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z. B. via Bilddatenbanken).)

Mame Diouf wa Hannover akishangiria bao dhidi ya Borussia Dortmund

Mlinzi wa Hannover Konstantin Rausch amesema hata hivyo kuwa ilikuwa kibarua kigumu kuidhibiti Borussia.

"Dortmund ni timu ngumu sana, lakini tuliweza kuwaweka katika mbinyo katika kipindi cha pili. Tulicheza mpira wa mashambulizi , na kutengeneza nafasi kadha za ushindi na mwishoni nilifurahi kwamba tuliweza kufanikiwa kupata sare. Kwa kuwa iwapo unapata nafasi za ushindi na huwezi kuzitumia , unapaswa kuridhika, kwa kuwa dakika zilikuwa zinayoyoma na kilichoweza kufanyika ni sare tu ya bao moja kwa moja".

Nayo VFB Stuttgart imeshindwa kwa mara nyingine tena kupata kile kilichotarajiwa kuwa nafasi ya mwanzo mpya wa kupata points tatu mara hii dhidi ya Bayer Leverkusen. Mwishowe Stuttgart na Bayer Leverkusen zilibidi kutosheka na sare ya mabao 2-2.

Stuttgart imebakia katika eneo la hatari ya kushuka daraja , wakati Leverkusen imeruka hadi katika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya Ujerumani Bundesliga.

Licha ya kwamba mashabiki 40,000 waliofika kuliona pambano hilo hawakuridhika na jinsi timu yao ya Stuttgart ilivyocheza, lakini pia kocha wa timu hiyo Bruno Labadia alikasirishwa na taarifa za baadhi ya vyombo vya habari hapa , kuhusiana na mwenendo wa timu hiyo wa kusua sua msimu huu.

Labadia afoka

Akionekana dhahiri kuwa amekasirishwa Labadia alifoka na kutoa maneno makali kwa vyombo vya habari akisema makocha wa timu za Bundesliga sio tambara la kufutia uchafu.

"Ulipofika wakati wa mapumziko ,Raphael alionyesha kuwa ana matatizo na aliomba, abadilishwe. Nataka kusema wazi kuwa , makocha katika Bundesliga sio "mapipa ya kutupia taka", za watu wote hapa. Kuna mipaka yake, na hata hapa Stuttgart, nilazima niwaeleze wazi. Sishangai , kwamba kila baada ya miezi michache kunakuwa na kocha mpya hapa, kama ilivyo hapa kutokana na hali ilivyo sasa. Kama kocha wa kawaida katika Bundesliga, ninapaswa kuuliza swali: Je naelekea katika njia , ambayo ni ya matatizo?, ambayo Stuttgart inapaswa kuelekea , na mimi je napaswa kuifuata?. Ama niseme, potelea mbali".

Ni maneno ya hasira ya kocha Bruno Labadia wa VFB Stuttgart, akilenga waandishi habari pamoja na uongozi wa Stuttgart.

Borussia Moenchngladbach imefanikiwa kusitisha msusuru wa kutoshindwa kwa timu iliyorejea msimu huu katika Bundesliga , Eintracht Frankfurt kwa ushindi wa mabao 2-0 jumapili na pia ni kipigo cha kwanza kwa timu hiyo.

Huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Moenchengladbach msimu huu baada ya michezo saba. Kikosi cha Lucien Favre kilihimili mashambulizi ya mara kwa mara ya Frankfurt na hatimaye kupata ushindi ambao mchezaji wa kati wa timu hiyo Tony Jantschke amesema ni wa kazi.

Haikuwa rahisi leo hii. Tulilazimika kupiga mipira ya mbali mingi. Hii sio aina yetu ya mchezo. Lakini wakati tukijaribu kucheza hivyo na kufunga mlango wetu, hakuna aliyeweza kuufungua wakati wote.

Matokeo haya yamekuja baada ya kazi ngumu tuliyoifanya leo na tumefurahi, kwamba tumeshinda kwa mabao mawili kwa bila.

Bayern yawania kufuta rekodi ya Dortmund

Bayern Munich huenda imeweza kufikia rekodi ya kushinda michezo mingi mwanzoni mwa msimu wa ligi ya Ujerumani , Bundesliga, lakini Bastian Schweinsteiger anasisitiza kuwa kikosi cha Bayern safari hii kinataka kuvunja rekodi ya Borussia Dortmund katika udhibiti wa ligi.

Winga kutoka Ufaransa Frank Ribbery alifanikiwa kuipatia Bayern Munich mabao yote mawili siku ya Jumamosi wakati Bayern ikinyakua ushindi wake wa saba katika ligi dhidi ya Hoffenheim.

Timu ya mwisho kupata ushindi mara saba mwanzoni mwa msimu, ilikuwa Mainz 05 katika msimu wa mwaka 2010/11, wakati Bayern Munich ilifanya hivyo mara ya mwisho katika msimu wa 1995/96, lakini katika misimu yote hiyo Dortmund iliibuka kidedea kwa kunyakua ubingwa, kama walivyofanya katika misimu miwili iliyopita.

Wachunguzi wa masuala ya soka hawaondoi basi uwezekano huo msimu huu , licha ya kuwa Borussia Dortmund hivi sasa iko nyuma ya Bayern kwa points tisa kama msimu uliopita baada ya michezo saba. Ni suala la kungoja na kuona.

El Classico, ni Messi na Ronaldo

Huko nchini Uhispania jana ilikuwa ile mechi iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka kote duniani, ya el Classico, kati ya Real Madrid na Barcelona. Washambuliaji wa timu hizo, Christiano Ronaldo wa Real na Leonel Messi wa Barcelona walikuwa tena kivutio kikubwa na wanaendelea na ushindani wao binafsi wa nani zaidi. Hakuna mshindi wala aliyesindwa katika mpambano wa jana. ulikuwa mpambano pia wa kupima nani anastajili kupata tuzo ya Ballon D'Or. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2, mabao ambayo yametiwa kimiani na washambuliaji hao wawili.

WARSAW, POLAND - JUNE 21: Cristiano Ronaldo of Portugal reacts during the UEFA EURO 2012 quarter final match between Czech Republic and Portugal at The National Stadium on June 21, 2012 in Warsaw, Poland. (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)

Cristiano Ronaldo wa Real Madrid

Kocha wa Real Jose Mourinho, aliwasifu Ronaldo na Messi. Si ruhusa kusema nani kati yao ni bora zaidi. Wanatoka katika sayari nyingine kabisa. Matokeo ni sahihi kwa mchezo huo. Kuna mambo ambayo tunapaswa kuyafanyia kazi, lakini leo tumeona mchezo safi.

Mlinzi wa Real Pepe lakini amedai Ronaldo alikuwa bora zaidi kuliko Messi. Ni wachezaji wawili bora kabisa, lakini kwa mtazamo wangu Cristiano ni zaidi kati yao. Kwangu mimi ni mchezaji bora duniani.

Barcelona's Lionel Messi (L) is congratulated by team mate David Villa after scoring his second goal against Spartak Moscow during their Champions League Group G soccer match at Nou Camp stadium in Barcelona, September 19, 2012. REUTERS/Gustau Nacarino (SPAIN - Tags: SPORT SOCCER)

Leonel Messi akishangiria bao

Kocha wa Barcelona Tito Vilanova , amesema kuwa jioni ya leo tulikuwa hatuna kikundi kizima cha walinzi wetu ambao ni chaguo la kwanza, lakini wachezaji waliochukua nafasi zao walifanya vizuri.

Matatizo ya ulinzi ya Barcelona yaliongezeka zaidi wakati mlinzi wa kulia Dani Alves alipotoka nje akichechemea baada ya kupata maumivu katika paja.

Maneno ya mkosaji

Huko Italia , Kocha wa AC milan Massimiliano Allegri amemlaumu refa na kusema timu yake ilicheza soka nzuri , katika matamshi ya kawaida baada ya kupata kipigo kutoka kwa mahasimu wao , na watani wao wa jadi katika mji wa Milan, Inter jana Jumapili.

Allegri ambaye timu yake imefanikiwa kujikingia points saba tu kutokana na michezo saba na wako points 12 nyuma ya viongozi wa ligi ya Serie A Juventus Turin na Napoli, walionekana kupapia kukamata manyasi wakati jahazi likionekana kuzama.

tunapaswa kufahamu pale tulipokwenda kombo, kwa mara nyingine tena tumeruhusu bao kutokana na mpira wa adhabu, ameongeza Allegri.

Ferguson asema kikosi chake kimeiva

Sir Alex Ferguson anaamini kuwa kikosi chake cha Manchester United kiko tayari kuongeza mbinyo dhidi ya viongozi wa ligi ya uingereza Premier League, Chelsea baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Newcastle jana Jumapili, katika uwanja wa St James' Park .

Viongozi wa ligi hiyo Chelsea hata hivyo walitoka nyuma baada ya kufungwa bao moja na Norwich City na kufanikiwa kuibamiza timu hiyo kwa mabao 4-1. Mabingwa Manchester City wako katika nafasi ya tatu baada ya kuipa kipigo Sunderland cha mabao 3-0, wakati Tottenham Hotspurs ilipata ushindi wake wa nne mfululizo wa mabao 2-0 dhidi ya Aston Villa.

Olympique Marseille imerejea kileleni katika ligi ya Ufaransa baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Paris St Germain licha ya juhudi kubwa za Slatan Ibrahimovich katika mchezo huo jana Jumapili.

Kocha atakiwa kuwa mkali

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew ametakiwa kuwa mkali kwa wachezaji wake , amesema hivyo rais wa Bayern Munich , Uli Hoeness kabla ya mchezo wa kufuzu kucheza katika fainali za kombe la dunia dhidi ya Ireland na Sweden.

Ujerumani itajitupa uwanjani kucheza na jamhuri ya Ireland katika uwanja wa Aviva mjini Dublin Ijumaa ijayo na kisha kuwakaribisha Sweden katika uwanja wa olympiki mjini Munich siku ya Jumanne Oktoba 16 wiki ijayo.

Hoeness amesema kuwa Loew ambaye ni mpole anapaswa kufikiri upya juu ya mtazamo wake huo kwa wachezaji wake na kuwa mkali kidogo katika juhudi za kuwafanya wajitume zaidi.

Kandanda ndio inayounganisha umma

Wakati huo huo mshambuliaji nyota wa Cote D'Ivoire Didier Drogba amesema leo kuwa anaamini kuwa mchezo wa mpira ni njia pekee ya kuwaunganisha watu wa nchi hiyo iliyokumbwa na vita. Timu ya taifa ina maana kubwa kwa nchi hii. Nafikiri kuwa leo hii, na natamka kwa tahadhari , kuwa ni kitu pekee ambacho kinaweza kuwaunganisha watu wa Cote D'Ivoire, Drogba amesema katika mahojiano na mtandao wa FIFA.

Chelsea's Didier Drogba reacts after scoring a goal against Barcelona during their Champions League semifinal first leg soccer match at Chelsea's Stamford Bridge stadium in London,Wednesday, April 18, 2012. (Foto:Matt Dunham/AP/dapd)

Didier Drogba

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ameongeza; na hapa namnukuu," ni kweli kwamba kuna michezo mingine nchini Cote D'Ivoire, lakini mchezo wa mpira kwa sasa ndio maarufu, na ni mchezo unaolileta taifa lote pamoja kwa mtazamo wangu", mwisho wa kumnukuu.

Kwa matamshi hayo ya Didier Drogba ndio sina budi kusema tumefikia mwisho mpenzi msikilizaji wa kuwaletea habari hizi za michezo kwa leo, jina langu ni Sekione Kitojo, hadi mara nyingine kwaherini.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / rtre / dpae

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman