Maafisa wa zamani wa radha kukata rufaa | Michezo | DW | 02.02.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Maafisa wa zamani wa radha kukata rufaa

Maafisa watatu wa riadha waliopigwa marufuku kujihusisha na maswala ya michezo huo kutokana na tuhuma za rushwa wamedai kuwa watakata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo - CAS

Maafisa hao ni Papa Massata Diack, ambaye ni mtoto wa rais wa zmani wa shirikisho la riadha duniani - IAAF Lamine Diack, Mrusi Valentin Balakh-nichev na Alexei Melnikov.

Maafisa hao walishtakiwa mnamo mwezi Desemba mwaka jana kwa kosa la ukiukaji wa sheria za kupambana na dawa za kuongeza misuli nguvu.

Diack na Balakhnichev, rais wa zamani wa shirikisho la riadha la Urusi na mweka hazina wa IAAF, walipigwa faini ya pauni 17,000 wakati kocha wa Urusi Melnikov alipigwa faini ya pauni 10,000.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Iddi Sessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com