1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Maafisa saba wa jeshi la Pakistan wauawa katika shambulizi

12 Mei 2024

Jeshi la Pakistan limesema leo kuwa takriban maafisa wake saba wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti karibu na mpaka wa Afghanistan

https://p.dw.com/p/4fl09
Mwanajeshi wa Pakistan na wa kundi la Taliban washika doria katika kivuko cha mpakani cha mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo mawili mnamo Agosti 21,2021
Mwanajeshi wa Pakistan na wa kundi la Taliban washika doria katika kivuko cha mkoa wa Khyber PakhtunkhwaPicha: AP Photo/dpa/picture alliance

Jeshi la Pakistan limesema kuwa katika shambulio la kwanza, kifaa cha mlipuko kililenga gari la kikosi cha kutegua mabomu katika eneo la Datta Khel jimboni Waziristan, Kaskazini mwa nchi hiyo jana Jumamosi. Baada ya mlipuko huo, washambuliaji hao walifyatua risasi.

Soma pia:Mashambulio ya Pakistan yaua watu kadhaa Afghanistan

Wanajeshi watano wa vikosi vya usalama waliuawa, na wawili kujeruhiwa. Katika shambulio la pili, wanamgambo walivamia kituo cha ukaguzi katika eneo la Mir Ali na kuwaua wanajeshi  wawili.

Mashambulizi ya kundi la Taliban yaongezeka nchini Pakistan

Pakistan imeshuhudia ongezeko la mashambulizi ya kundi la Taliban la nchi hiyo tangu wenzao katika upande wa Afghanistan waliponyakua mamlaka nchini Afghanistan mnamo mwaka 2021.

Soma pia:Taliban: Pakistan imefanya mashambulizi ya anga Afghanistan

Mashambulizi ya hivi karibuni zaidi yanajiri siku chache baada ya wanamgambo kulipua bomu katika shule ya wasichana iliyoko Kaskazini mwa Waziristan, eneo linalojulikana kuwa kitovu cha shughuli za wanamgambo wa makundi ya itikadi kali.