Maadhimisho ya miaka 60 ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 22.05.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Maadhimisho ya miaka 60 ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani

default

Rais Horst Köhler

Rais Horst Köhler  wa Ujerumani amesema kwamba Ujerumani imestawi kuwa  nchi  yenye  uwazi na ya kimataifa katika historia yake ya  miaka  60.

Rais Köhler amesema hayo mjini Berlin leo katika maadhimisho  ya miaka 60 tokea kuundwa  kwa shirikisho la Jamhuri  ya  Ujermani.

Amesema katika miaka 60 iliyopita Ujerumani limekuwa taifa lenye uwazi kwa dunia  .Ameeleza kuwa Ujerumani imeshiriki katika juhudi za kuunda jumuiya   za Umoja  wa Ulaya  na pia imeshsiriki  katika kuweka  malengo  ya kisiasa ya  jumuiya hizo.

Amesema  Ujerumani imekabiliana na uhalifu  uliotendwa na mafashisti  na imefikia maridhiano na taifa la kiyahudi.

Rais  Köhler  ameeleza  kuwa wajerumani  wamejifunza  kutokana  na historia  na  ndiyo sababu kwamba wakati  wote  itapinga maovu ya chuki dhidi  ya wayahudi,ubaguzi ,na chuki dhidi  ya wageni.

Juu ya katiba ya Ujerumani   iliyoweka msingi  wa demokrasia nchini, rais Köhler  amesema  kuwa hati hiyo ni mwenge wa  wa uhuru.Ameeleza kuwa katiba hiyo  iliwapa  wajerumani wa upande wa mashariki, matumaini.

Kuhusu  medani ya kimataifa rais Köhler amesema kuwa Ujerumani imeshirikiana na nchi inayofungamana nazo katika kuletekeleza  majukumu ya  ya kimataifa.

Imesaidia katika kutatua  migogoro mbalimbali duniani  na  kwamba Ujerumani  imetoa mchango wake katika  kulinda amani na haki za binadamu   duniani.Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com