1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 wakamata mji mashariki mwa Kongo

Lilian Mtono
8 Desemba 2023

Waasi wameukamata mji wa Mushaki, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya mapigano makali na jeshi, ambalo linaendeleza juhudi za kuyadhibiti makundi ya waasi baada ya vikosi vya kulinda amani kuondoka.

https://p.dw.com/p/4ZujV
Wanajeshi wa Burundi wanaohudumu kwenye kikosi cha Afrika Mashariki nchini Kongo.
Wanajeshi wa Burundi wanaohudumu kwenye kikosi cha Afrika Mashariki nchini Kongo.Picha: Alexis Huguet/AFP

Maafisa wa kijeshi na raia wa mji huo wameliambia shirika la habari la AP kwamba, wanamgambo wa M23 wameingia Mushaki na kuvidhibiti vituo muhimu vya kijeshi, hatua iliyowafanya wengi kukimbia.

Soma zaidi: Waasi wa M23 wachukua udhibiti wa mji wa kimkakati karibu na Goma

Hata hivyo, jeshi hilo limesema limetumia vikosi vyake kuwadhibiti wanamgambo hao kabla ya kufanikisha azma yake kwenye mji huo. 

Mji wa Mushaki ni kitovu cha usafirishaji hadi kwenye miji mikubwa ya jimbo la Kivu, mashariki mwa Kongo.