LUSAKA:Zambia kuzindua reli kuelekea Msumbiji | Habari za Ulimwengu | DW | 22.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUSAKA:Zambia kuzindua reli kuelekea Msumbiji

Rais Levy Mwanawasa wa Zambia ataongoza uzinduzi wa mpango wa reli itakayo unganisha nchi yake na pwani ya nchi jirani.

Waziri anaehusika na maswala ya mashariki wa Zambia Lameck Mangani amesema kwamba rais Mwanawasa ataungana na marais Armando Guebuza wa Msumbiji na Bingu Wa Mutharika wa Malawi katika mji wa Chipata siku ya ijumaa katika uzinduzi rasmi wa ujenzi wa reli yenye kilomita 26.

Mpango huo utagharimu kiasi cha Euro milioni 8.9 na unatarajiwa kuiunganisha miji ya Chipata nchini Zambia na mji wa Mchinji nchini Malawi ambako kuna njia inayo elekea katika mji wa pwani wa Nacala nchini Msumbiji.

Viongozi hao pia watajumuika katika sherehe za jamii ya Chewe ilinayopatikana katika nchi zote tatu za Zambia, Malawi na Msumbiji.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com