Lufthansa yawasilisha kesi ya mgomo mahakamani | Masuala ya Jamii | DW | 10.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Lufthansa yawasilisha kesi ya mgomo mahakamani

Shirika la ndege la Ujerumani - Lufthansa limewasilisha kesi mahakamani dhidi ya wahudumu wa ndege hiyo ili kumaliza mgomo wa siku nne huku chama cha wafanyakazi hao kikitangaza mipango ya kuendelea na mgomo wao

Chama hicho cha wafanyikazi UFO kimesema Safari zote za ndege za mbali na kadri nchini Ujerumani zitakumbwa na mgomo huo kuanzia Jumatano hadi Ijumaa.

Mapema leo Shirika hilo la ndege lilisema limewasilisha kesi katika mahakama za Dusseldorf na Darmstadt ili uamuzi ufanywe kuhusu mgomo huo unaoongozwa na wahudumu wa ndege ,ambao umechukua muda mrefu ambao haujawahi kushuhudiwa.

Lufthansa ililazimika kufutilia mbali safari za ndege 136 siku ya Jumanne baada ya wafanyikazi wake kugoma kuhusiana na malipo na hatua ya shirika hilo kuongeza umri wa kustaafu.

Chama cha kutetea wafanyikazi hao UFO kinachowakilisha wafanyikazi elfu 19000 kimesisitiza kuendelea kwa mgomo huo baada ya kukataa nyongeza mpya waliyopewa na shirika hilo la ndege.

Chama hicho cha wafanyikazi kimelenga viwanja vya ndege vya Frankfurt,Munich and Dusseldorf , viwanja ambavyo ni muhimu kwenye mtandao wa shirika hilo la ndege.

Kwa mujibu wa shirika hilo la ndege kati ya safari zitakazo futiliwa mbali siku ya Jumanne, 126 ni za kutoka bara moja hadi nyingine,huku 10 zikiwa za ulaya.

Deutschland Lufthansa Streik Lange Warteschlangen

Maelfu ya abiria waathirika na mgomo

Siku ya Jumatatu chama hicho cha wafanyikazi kilikataa nyongesa ya awamu moja kwa wanachama wake wa Euro 1000 sawa na dola elfu 1,075 hadi Euro 3000 na pia kubadilishwa kwa pendekezo la Lufthansa la awali la umri wa kustaafu kutoka umri wa miaka 55 hadi 56.Chama hicho kimesema haya ni mabadiliko machache mno.

Msemaji wa shirika la Lufthansa amesema wamewasilisha kesi yao kwa kuzingatia

matakwa ya wafanyikazi hao ambayo anasema sio dhahiri na yasiyoweza kutekelezwa chini ya sheria za wafanyikazi nchini Ujerumani.Naye kiongozi wa muungano huo wa wafanyikazi Nicoley Baublies amejibu matamshi hayo kwa kusema kuwa chama chao kitaendelea na mgomo hadi Ijumaa.

Chama cha wafanyikazi hao kinataka wahakikishiwe malipo ya uzeeni kwa wafanyikazi wake 19000 ikiwa watastaafu mapema hiii ikiwa kati ya matakwa yao kwenye mgomo huu .Chama hicho kimesema leo kuwa mapato ya shirika hilo kabla ya ushuru yaliongezeka kwenye makadirio yake ya mwaka.

Maelfu ya wasafiri wameathirika kufikia sasa kufuatia kufutwa kwa mamia ya safari zao.Lufthansa imedhibitisha leo kuwa safari zote kutoka Ujerumani zitatatizwa kuanzia saa kumi alfajiri siku ya Jumatano hadi usiku wa manane siku ya Ijumaa.

Mwandishi:Bernard Maranga/DPA/AP/AFP

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com