LONDON.Bomu lililotegwa kwenye barua lalipuka, mmoja ajeruhiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 05.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON.Bomu lililotegwa kwenye barua lalipuka, mmoja ajeruhiwa

Bomu lililotegwa ndani ya barua limelipuka na kumjeruhi mwanamke mmoja katika ofisi moja katikati ya mji wa London.

Mwanamke huyo amelazwa katika hospitali moja mjini humo.

Polisi wamesema kwamba eneo la barabara ya Victoria katikati ya mji wa London liliwekwa chini ya ulinzi baada ya kupokea taarifa za tahadhari kuhusu kifurushi kilichoshukiwa.

Polisi wa kupambana na ugaidi wa kikosi cha Scotland Yard wanaendesha uchunguzi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com