1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Loew atafakari kuhusu corona, Neuer aongoza mchango

Deo Kaji Makomba
19 Machi 2020

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew amezungumzia tafakari yake kutokana na hatari inayoendelea kuikabili dunia kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona vinavyoendelea kuua maelfu ya watu.

https://p.dw.com/p/3ZiT4
Deutschland - Pressekonferenz Joachim Löw vor dem Spiel Deutschland - Nordirland
Picha: picture-alliance/dpa/U. Anspach

Wakati kocha Mkuu huyo akitoa tathimini yake kuhusiana na janga hilo kwa upande wake nahodha wa timu hiyo ya taifa ya Ujerumani, Manuel Neuer, anaongoza kampeni ya uchangishaji pesa kwa ajili kuwasaidia watu mbalimbali katika jamii, walioathirika na virusi hivyo vya Corona ambavyo Shirika la Afya duniani, WHO, limevitangaza virusi hivyo kuwa ni janga la kimataifa.

Akizungumza mbele ya viongozi wa Shirikisho la kandanda nchini Ujerumani, DFB, katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano tarehe (18.03.2020), Loew alisema kuwa ameguswa na athari za virusi vya Corona na kuongeza kuwa siku kadhaa zilizopita amekuwa katika kutingwa na mawazo hasa kutokana na janga hili linalozidi kuitikisa dunia.

Kwa kuzingatia ushauri wa sasa wakati huu wa janga la virusi vya Corona, Shirikisho la soka la Ujerumani lilimtambulisha Rais Fritz Keller huko Frankfurt wakati Kocha Loew na mkurugenzi wa DFB Oliver Bierhoff wakizungumza kutoka Freiburg na Munich kwa mpangilio. Waandishi wa habari pia waliuliza maswali kupitia teknolojia ya vidio.

Kuahirishwa kwa michuano ya Euro ya mwaka huu wa 2020 hadi 2021 ulikuwa ni uamuzi sahihi kabisa, uamuzi bila njia mbadala," alisema Loew.

Mpira wa miguu uko nyuma, mambo mengine sasa ni muhimu zaidi. Alisema pia kuwa, "virusi vya Corona vinaikabili dunia. Hesabu yangu kwa sasa ni kuhusu familia na marafiki ni wapi ninaweza kuwasaidia watu wanaonizunguka? Majanga ya kimazingira yalitugusa mara kwa mara. Na sasa tumepata uzoefu fulani ambao umemuathiri kila mmoja na binadamu wote."

Na kuahirishwa kwa ligi ya Bundesliga hadi Aprili 2 na usajili wa dirisha dogo wa kimataifa wa mwezi Machi umechakaa. Loew na Wajerumani hawatakuwa ha jinsi hadi walau kufikia mwezi Juni na hata itategemea na janga hilo la virusi vya Corona.

Neuer aongoza mchango kusaidia jamii

Katar | Manuel Neuer im Trainingslager
Manuel Neuer, nahodha na kipa wa timu ya taifa ya UjerumaniPicha: Getty Images/Bongarts/A. Grimm


Wakati huo huo nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neur aliwataka mashabiki wa kandanda nchini humu kuchangia ili kuisaidia jamii iliyoathirika na virusi vya Corona, baada ya wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani kuingia mifukoni ili kuonyesha mfano katika zoezi la kuchangia.

"Yatupasa kuangalia kutoka kwa kila mmoja wetu kwa kipindi hiki. Tulikuwa pia na mawazo yetu na kuchangia euro milioni 2.5 sawa na dola milioni 2.7 kwa nia njema." Alisema Neuer mwenye umri wa miaka 33 katika vidio yake kwenye mtandao wa Instagram wa timu ya taifa ya Ujerumani."

Sisi sote ni timu kubwa, sio tu ndani ya uwanja bali pia katika jamii yetu," alisema. "Unatambua hilo kwa nyakati kama hizi."

Mlindamlango huyo wa klabu ya Bayern Munich aliungana katika vidio na wachezaji wenzake Joshua Kimmich na Leon Goretzka, mchezaji wa klabu ya Moenchengladbach, Mathias Ginter, mchezaji Lukas Lukas Klostermann anayeichezea RB Leipzig, Robin Koch na Luca Waldschimidt wanaochezea klabu ya Freiburg pamoja na Jonathan Tah anayechezea timu ya Bayer Leverkusen.

"Tunapaswa sote kuwa makini katika majukumu yetu na kuonyesha mshikamano kuanzia sasa," alisema Kimmich ambaye aliwashukuru wale wote waliojaliwa kuchangia na wataalamu waliowezesha kuwa utamaduni wa kujali unaendelea kubaki daima.

Kwa upande wake mchezaji Goretzka alisema kuwa soka limesimama kwa muda lakini afya ni muhimu zaidi
"Hiyo ni sawa. Tunasimama mbele ya matatizo makubwa ya kijamii yaliyotuathiri sisi sote na sio tu kwa  kizazi cha wazee."

Naye mchezaji Matthias Ginter aliongeza kusema, "Wacha tuonyeshe ishara ya kwamba tunasimama pamoja katika nyakati hizi za shida."

(AFPA)