1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liverpool yasherehekea ubingwa mitaani mjini Liverpool

Sekione Kitojo
3 Juni 2019

Wachezaji wa Liverpool ya England walisherehekea ubingwa wao wa Champions League na maelfu  ya  mashabiki  wa Liverpool jana  Jumapili (02.06.2019)wakati wakilionesha kombe lao na kulipitisha mitaani katika basi la wazi.

https://p.dw.com/p/3Jirw
UEFA Champions League Triumphfahrt FC Liverpool
Picha: Reuters/P. Noble

 Akiwa  katika  moja  kati  ya mabasi  hayo, shujaa  wa  fainali  hiyo  Divock Origi mwenye  asili ya  Kenya  amesema  ni  fahari  kuitwa  "lejendari  wa  Liverpool", kwa  jukumu  lake  lililosababisha  taji  hilo  kutua mjini  Liverpool. Divock  alisema

UEFA Champions League Triumphfahrt FC Liverpool
mabingwa wa Ulaya LiverpoolPicha: Getty Images/N. Roddis

"Ni vizuri kufahamu  hilo. Ni heshima kubwa. tunafahamu  Liverpool ina  maana  gani kwa dunia kama  klabu, kama  klabu  ya  mpira, kwa hiyo  nafikiri  tuna furaha  kwamba  watu  wanatoa  matamshi  kama hayo."

Mashabiki  wa  Liverpool walifyatua  fashifashi  na  kuimba  siku nzima  katika  mji huo  ambao  ulikuwa  na  rangi  nyekundu  kila mahali. Wachezaji  kama  Mo Salah, kocha  Juergen Klopp, mlinzi Virgil van Dijk  na  wengine  walishiriki katika  shehere hizo  kubwa, wakilionesha  kombe  wakiwa juu  ya  basi. Liverpool iliishinda Tottenham Hotspur  pia  ya  England  kwa  mabao 2-0  katika  fainali ya  Champions League mjini  Madrid  siku  ya  Jumamosi.

UEFA Champions League Finale | Tottenham Hotspur v FC Liverpool Joel Matip
Matip (kulia na Xherdan Shaqiri (kushoto) wakifurahia kunyakua kombe la Champions League barani UlayaPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Wakati  huo  huo  mchezaji  nguli  wa  kandanda  wa  Ujerumani Franz Beckenbauer  amesema  leo  kwamba  anataka  kumuona kocha  wa  Liverpool  Juergen Klopp katika  benchi  la  ufundi la Bayern. Wakati  Ujerumani  ikisherehekea  mafanikio  ya  Klopp katika  champions league  siku  ya  Jumamosi, Beckenbauer ameliambia  gazeti  la  Bild  kwamba  anataka  sana  kumuona  kocha huyo wa  zamani  wa  Borussia  Dortmund  akijiunga  na  mabingwa wa  Bundesliga , Bayern Munich.

UEFA Champions League Finale | Tottenham Hotspur v FC Liverpool Mo Salah
Kocha Klopp, (kulia ) akiwa na mchezaji wake Mo SalahPicha: Reuters/T. Melville

"Sitaka  kitu  kingine  zaidi  ya  kumuona  Klopp akija  Bayern siku moja, itakuwa  kitu  kizuri  sana," amesema  Beckenbauer mwenye umri  wa  miaka  73, ambaye  alishinda  ubingwa  mara tano wa Bundesliga  na  Bayern  akiwa  kama  mchezaji  na  kocha. Ubingwa wa  kwanza  wa  Klopp  wa  Champions League ulisababisha sherehe  kubwa  katika  vyombo  vya  habari  za  michezo  nchini Ujerumani.

Na  pia  juhudi  za  Bayern Munich za kupata saini  ya  mshambuliaji wa  Manchester City Leroy Sane  zinaonekana  kugonga  mwamba, rais  wa  klabu  hiyo Uli Hoeness amenukuliwa  akisema  katika ripoti  leo Jumatatu.

Premier League 31. Spieltag | Manchester United vs. Manchester City
Mshambuliaji wa Manchester City Leroy SanePicha: Imago Images/PA Images/M. Egerton

"Unalazimika  kuwa  kidogo  na  shaka. Kuna  uwezekano  kwamba haitawezekana. Ni  kuhusu wenda  wazimu  wa malipo ya  uhamisho," gazeti  la  michezo  la  Kicker  lilimnukuu Hoeness. Kwa  mujibu wa ripoti  za  vyombo  vya  habari, Manchester City inafanya  juhudi mpya  kurefusha  mkataba  wa  mchezaji  huyo  wa  kimataifa  wa Ujerumani  mwenye  umri  wa  miaka  23.