1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liverpool hawashikiki

16 Desemba 2019

Liverpool wamefungua mwanya wa pointi kumi baina yao na timu iliyo kwenye nafasi ya pili Leicester City. Hii ni baada ya hao the Reds kupata ushindi wa mbili bila walipokwaana na Watford Jumamosi.

https://p.dw.com/p/3UuQD
Fussball Champions League l Red Bull Salzburg vs Liverpool l Tor 0:2 - Mohamed Salah Jubel
Picha: Reuters/J. Sibley

Mo Salah aliyekuwa mfungaji wa mabao hayo mawili kisha Leicester wakatoka sare ya bao moja na Norwich City.

Baada ya kuwalaza Tottenham Hotspur na Manchester City katika mechi zao mbili zilizopita Manchester United walilazimisha sare ya bao moja na Everton uwanjani Old Trafford. Huyu kocha wa United Ole Gunnar Solksjaer akimzungumzia mshambuliaji chipukizi wa klabu hiyo Mason Greenwood aliyefunga goli la kusawazisha na kuwapa United pointi moja.

"Wachezaji wanaopitia mafunzo ya mpira katika klabu hii wanaelewa ni kitu gani kinachotakikana kwa wewe kuwa mchezaji wa Manchester United na Mason Greenwood ni mfano mzuri," alisema Solskjaer.

Arsenal walipewa funzo la soka uwanjani kwao na Manchester City

Chelsea walifungwa mdomo na Bournemouth moja bila halafu Jose Mourinho na Tottenham Hotspur yake wakatoa ushindi wa mbili moja ugenini dhidi ya Wolverhampton Wanderers na baada ya hapo Manchester City wakaishindilia Arsenal mabao matatu bila jawabu huko Emirates.

Fußball FC Arsenal vs Manchester City | Mesut Özil Auswechslung
Mesut Özil akionyesha hasira baada ya kutolewa uwanjani katika mechi na Man CityPicha: Getty Images/AFP/B. Stansall

Na licha ya ushindi huo mkubwa dhidi ya Arsenal kocha wa Man City Pep Guardiola amesema kucheza na klabu hiyo ya London ilikuwa ni changamoto.

"Kawaida Arsenal wana mtindo wa kipekee wa kucheza kwa hiyo ukiwaacha wacheze wana wachezaji wazuri wa kucheza vyema, wachezaji kama Pepe, Aubameyang na Lacazette, Arsenal ni changamoto kubwa kwa timu yoyote," alisema Guardiola.

Liverpool sasa wanaiongoza ligi hiyo kwa pointi arubaini na tisa wakifuatiwa na Leicester walio na pointi thelathini na tisa halafu Manchester City katika nafasi ya tatu wana pointi thelathini na tano.