Liverpool watabeba ubingwa wa ligi bila kupoteza mechi? | Michezo | DW | 13.01.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Liverpool watabeba ubingwa wa ligi bila kupoteza mechi?

Miaka 30 ya kusubiri kushinda kombe la ligi imekuwa mingi sana kwa Liverpool na vijana wa kocha Jurgen Klopp wanaonekana kuwa katika harakati za kumaliza ukame huo haraka iwezekanavyo

Miaka 30 ya kusubiri kushinda kombe la ligi imekuwa mingi sana kwa Liverpool na vijana wa kocha Jurgen Klopp wanaonekana kuwa katika harakati za kumaliza ukame huo haraka iwezekanavyo kutokana na mwanzo wao bora kabisa wa msimu katika ligi tano kubwa za Ulaya. Waliwazala Tottenham Hotspur 1 – 0 mwishoni mwa wiki ikiwa ni ushindi wao wa 20 kwenye ligi katika mechi 21 msimu huu. Alipoulizwa kuhusu rekodi ya kuwa na mwanzo bora kabisa wa msimu, Klopp alijibu

Lakini hatukuwaza hata kwa sekunde moja kabla, na baada ya mechi mtu akanikumbusha kuhusu hilo, kwa hiyo inapendeza sana lakini kama itabaki hivyo nnaweza kufikiria juu ya hilo katika miaka mitano ijayo. lakini kwa sasa, nnaweza tu kusema kuwa tulijaribu kufanya tuwezalo na tulicho nacho ili kuweka msingi wa sehemu iliyobaki ya msimu. msimu bado mrefu na tuna mechi nyingi ngumu za kucheza, inayofuata ni Man United na ni ngumu. tunapaswa kujiandaa vyema.

Liverpool wanaongoza kileleni na pengo la pointi 14 mbele ya nambari mbili Manchester City na wana mechi moja ya ziada ya kucheza. City waliifunga Aston Villa 6 -1 katika mechi ambayo Sergei Aguero alifunga hat trick na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kigeni katika Premier League kufumania nyavu mara nyingi kabisa. Amefunga mabao 177 katika Premier League katika mechi 255 za ligi. Amívunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thiery Henry ambaye ana 175 katika mechi 258