Liverpool waibamiza Chelsea Anfield | Michezo | DW | 15.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Liverpool waibamiza Chelsea Anfield

Liverpool waliuchukua tena uongozi wa Ligi Kuu ya England baada ya kuishindilia Chelsea mabao mawili kwa bila uwanjani Anfield washambuliaji hatari wa hao the Reds Sadio Mane na Mohammed Salah wakifunga mabao hayo.

Lililozungumziwa sana katika mechi hiyo lilikuwa ni goli la Salah alilofunga kwa mkwaju mkali kutoka yadi ishirini na tano.

Lakini kabla ya mechi hiyo kulikuwa na kanda ya vidio iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha mashabiki wa Chelsea wakiimba nyimbo za kibaguzi dhidi ya mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salah na jambo hilo halikumfurahisha meneja Jurgen Klopp wa Liverpool.

"Ni jambo linalokera. Ni mfano mwengine wa kitu ambacho hakistahili kufanyika, ni ishara nyengine kwamba kuna jambo ambalo haliko sawa mahali. Unapofanya kitu kama hicho haustahili kukubaliwa kuingia tena katika uwanja wa mpira," alisema Klopp.

Liverpool sasa wanaongoza kwa pointi 85 huku Manchester City wakiwa kwenye nafasi ya pili na pointi 83 ingawa Liverpool wamecheza mechi moja zaidi ya Liverpool huku kukiwa kumesalia mechi tano tu ligi hiyo kufika ukingoni.