Ligi kuu ya kandanda England yapamba moto | Michezo | DW | 16.02.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ligi kuu ya kandanda England yapamba moto

Arsenal na Tottenham Hot Spurs zilishinda michezo yake kwa mabao 2-1, Arsenal ikiikandika Leicester City viongozi wa ligi ya Uingereza kwa sasa, na Spurs wakiiangusha chini Man City kwa idadi hiyo hiyo ya mabao

Na kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini anaweza kukabiliwa na hatua kali kutoka chama cha soka nchini Uingereza baada ya raia huyo kutoka Chile kumkosoa refa Mark Clattenburg baada ya timu yake kushindwa hapo jana dhidi ya Tottenham.

Pellegrini alimshutumu refa Clattenburg kwa kutaka kuwazawadia penalti Spurs na kutoa tathimini kali dhidi ya refa huyo kutokana na jinsi alivyoendesha mchezo mwingine na Tottenham mwezi Septemba mwaka jana.

Kikosi cha kocha nyota Juergen Kloop cha Liverpool kiliirarua Aston Villa jana Jumapili kwa mabao 6-0 na kuimarisha nafasi yake kuelekea katika nfasi za kucheza kombe la Ulaya.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / dpae /zr /
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com