1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen uso kwa uso na Rangers ligi ya Ulaya

Deo Kaji Makomba
6 Agosti 2020

Kivumbi cha ligi ya Ulaya kinatarajia kuendelea tena Alhamisi na Ijumaa huku kukishuhudiwa timu kadhaa zikishuka dimbani kupepetana katika mechi za mzunguko wa 16.

https://p.dw.com/p/3gY26
Fußball: Bundesliga | Bayer Leverkusen - 1. FC Union | 1:0
Kelvin Volland wa Bayer Leverkusen mwenye jezi namba 31 akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga baoa katika moja ya mechi ya Bundesliga.Picha: Getty Images/Bongarts/C. Koepsel

Bayer Leverkusen ya Ujerumani bado wana nyota wao Kai Havertz licha ya kuwepo na  uvumi wa mchezaji huyo kuhama. Rangers inarudi kwa msimu wa 2019-20 katika Ligi ya Ulaya licha ya kwamba tayari ilishacheza mechi yake ya kwanza 2020-21 katika mchezo wa ligi ya Scotland, ilipoipiga Aberdeen bao 1-0 Jumamosi.

Timu ya Roma iko katika kiwango  kizuri baada ya kushinda mechi saba kati ya nane za mwisho katika ligi ya Serie A, ikiwa ni pamoja na ushindi wa 3-1 dhidi ya Juventus Jumamosi.

Sevilla haijafungwa katika mashindano yoyote tangu mwezi Februari na imekuwa na wiki tatu za kupumzika tangu msimu wa ligi ya Uhispania kumalizika, ikilinganishwa na siku tano kwa Roma.

Timu ya Wolves ilikosa kufuzu Ligi ya Ulaya kupitia Ligi ya Uiingereza, lakini bado wanaweza kuiga mbio zao bora kabisa za Ulaya kutoka 1972, wakati wapolifika fainali ya Kombe la UEFA.

Olmpiakos imeona upinzani mwingi wa Kiingereza msimu huu baada ya kuitupa Arsenal nje ya Ligi ya Ulaya na kucheza naTottenham kwenye Ligi ya Mabingwa.

Nayo timu ya Basel inakusudia kuendeleza wimbi lake la ushindi kutoka katika mzunguko wa kwanza lakini inaweza kuwa iliyoathiriwa na uchovu baada ya kumaliza msimu wa ligi ya Uswizi pamoja na michezo Ijumaa na Jumatatu.

Frankfurt haijacheza mchezo wa ushindani tangu Juni 27 lakini walitoka sare 1-1 na Monaco katika mechi ya kirafiki Jumamosi iliyopita.

Manchester United na Inter Milan zimefanikiwa kutinga kwenye robo fainali ya Ligi ya Ulaya Jumatano baada ya kurejea tena kwa michuano hiyo bila ya kuwa na mashabiki uwanjani kufuatia mlipuko wa virus vya Corona.

Chanzo: AP