1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni siku ya kupambana na ugonjwa wa Malaria

25 Aprili 2019

Leo tarehe 25 ni siku ambapo ulimwengu unaadhimsiha Siku ya kupambana na ugonjwa wa Malaria. Hali ya ugonjwa huo wa malaria katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hasa katika jimbo la Kivu kusini hairidhishi.

https://p.dw.com/p/3HQRB
Medizin Forschung l Weltweit erste Malaria-Impfkampagne l Mücke der Gattung «Anopheles gambiae»
Picha: picture alliance/dpa/S. Morrision

Leo tarehe 25 ni siku ambapo ulimwengu unaadhimsiha Siku ya kupambana na ugonjwa wa Malaria. Hali ya ugonjwa huo wa malaria katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hasa katika jimbo la Kivu kusini hairidhishi. Kulingana na ripoti ya shirika la madaktari wasio na mipaka MSF, ugonjwa huo umeathiri watoto zaidi ya 1,600 hasa katika wilaya ya Fizi. Aidha, kuna changamoto nyingi kuhusiana na matumizi ya vyandarua. Mapema wiki hii Shirika la afya duniani, WHO kwa mara kwanza katika historia lilizindua programu ya majaribio ya chanjo ya Malaria kwa watoto nchini Malawi. Chanjo hiyo ijulikanayo kama RTS,S ni ya kwanza duniani ambayo imeonyesha kutoa kwa sehemu kinga ya malaria kwa watoto. Mratibu wa WHO katika programu hiyo Mary Hamel alisema Malaria bado ni janga kubwa linalosababisha zaidi ya vifo vya watoto 250,000 barani Afrika kila mwaka. Malawi, Ghana na Kenya zimeteuliwa kufanyiwa majaribio ya chanjo hiyo mpya iliyochukua miaka 30 kutengenezwa