Leo ni Leo! | Michezo | DW | 26.06.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Leo ni Leo!

Mashindano ya Kombe la Dunia kwa wanawake yanaanza leo

default

FIFA Kombe la dunia 2011

Mashindano ya Kombe la dunia kwa wanawake yanaanza hii leo nchini Ujerumani. Maelfu ya mashabiki wanatarajiwa kumiminika hii leo katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin katika mechi ya ufunguzi kati ya timu mwenyeji, Ujerumani dhidi ya Canada.

Weltmeisterpokal der Frauenfussball-WM 2011

Kombe lenyewe linalowania

Timu ya taifa ya Ujerumani inashiriki mashindano haya ikiwania kulinyakuwa kwa mara ya tatu taji hilo. Ufaransa itaonana na timu mojawapo kati ya mbili kutoka Afrika, Nigeria zote zikiwa kwenye kundi A. Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Silvia Neid anasema wanahitaji mwanzo mzuri katika mashindano haya, licha ya kuwa mpambano wa leo utakuwa mkali.

Frauen Nationalmannschaft Birgit Prinz

Birgit Prinz uwanjani

Timu hiyo ya wanawake ya Ujerumani inaongozwa na Birgit Prinz mwenye umri wa miaka 33, ambaye amefanikiwa mpaka sasa kuifungia Ujerumani mabao 128, na kulinyanyua taji la mashindano haya mjini Shanghai China miaka 4 iliyopita.

Mwandishi: Maryam Dodo Abdalla
Mhariri:Kitojo,Sekione