1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Laurent Gbagbo akataa kung'atuka madarakani

P.Martin/rtre4 Januari 2011

Wapatanishi wa Kiafrika wameondoka Cote d'Ivoire bila ya hiyo jana kufanikiwa kumshinikiza Laurent Gbagbo kumkabidhi madaraka mpinzani wake Alassane Ouattara.

https://p.dw.com/p/QmYl
Opposition leader Alassane Ouattara, right, with United Nations's envoy to Ivory Coast, Choi Young-jin, left, prior to a meeting at the Golf hotel in Abidjan, Ivory Coast, Thursday, Dec. 9, 2010. The U.N. Security Council is ready to take targeted measures against people who try to upset the peace process or violate human rights in Ivory Coast. The international body is also calling on all sides to respect the electoral victory of opposition presidential candidate Alassane Ouattara. (AP Photo/Thibault Camus)
Alassane Ouattara(kulia) pamoja na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Cote d'Ivoire,Choi Young-jin.Picha: AP

Leo,viongozi hao watakutana na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alie pia mwenyekiti wa hivi sasa wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi ECOWAS.

Marais wa Benin,Sierra Leone na Cape Verde wakiwakilisha ECOWAS na Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga kwa niaba ya Umoja wa Afrika walikwenda Cote d'Ivoire ambako walikuwa na mazungumzo pamoja na Gbagbo kabla ya kuonana na Ouattara.

ECOWAS imetishia kutumia nguvu za kijeshi ikiwa Gbagbo atakataa kumkabidhi madaraka Ouattara anaetambuliwa na jumuiya ya kimataifa kuwa ni mshindi wa uchaguzi uliofanyika mwezi wa Novemba.Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari,Gbagbo ameahidiwa na viongozi hao wa Kiafrika usalama wake na kwamba hatoshtakiwa ikiwa ataondoka kwa amani.