1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lampard apigwa kalamu Chelsea

25 Januari 2021

Uongozi wa Frank Lampard wa miezi 18 katika klabu ya Chelsea umefikia mwisho baada ya klabu hiyo ya London magharibi kumfuta kazi huyo mchezaji wao wa zamani.

https://p.dw.com/p/3oNsR
Chelsea manager Frank Lampard
Picha: imago images/PA Images/A. Rain

Katika msimu wake wa kwanza aliisaidia Chelsea kumaliza katika mojawapo ya nafasi za Champions League ila kwa kuwa klabu hiyo inashikilia nafasi ya 9 kwenye msimamo kwa sasa, mmilki Roman Abramovich amelazimika kuchukua hatua.

Chelsea imesema haitatoa taarifa nyengine yoyote hadi pale mrithi wa Lampard atakapotangazwa. Wachambuzi wanasema kocha wa zamani wa Borussia Dortmund na PSG Thomas Tuchel ndiye anayetarajiwa kuichukua nafasi hiyo.