LADY LAKE : Kimbunga chauwa watu 20 Florida | Habari za Ulimwengu | DW | 04.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LADY LAKE : Kimbunga chauwa watu 20 Florida

Eneo la kati la jimbo la Florida nchini Marekani limekumbwa na kimbunga na dhoruba za upepo na kusababisha kupotea kwa maisha ya watu 20 na mamia ya nyumba kuharibiwa.

Wakaazi karibu 20,000 hawana huduma ua umeme. Rais George W. Bush wa Marekani ametangaza maeneo manne ya jimbo hilo kuwa ya maafa na kuruhusu kutolewa kwa msaada wa serikali kurudisha maisha ya watu katika hali ya kawaida.

Kimbunga hicho kimepiga wakati wa alfajiri ambapo watu wachache walikuwa macho kuweza kusikia matangazo ya tahadhari yaliotolewa kwa muda mfupi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com