Kugunduliwa kwa kaburi la halaiki eneo la Tana River nchini Kenya | Matukio ya Afrika | DW | 18.09.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kugunduliwa kwa kaburi la halaiki eneo la Tana River nchini Kenya

Kaburi la halaiki linadaiwa kugunduliwa katika eneo la Tana River nchini Kenya, mkoa ambao umegubigwa na mapigano ya kikabila kati ya makabila ya Wapokomo na Waorma ambayo yamesababisha watu zaidi ya 100 kupoteza maisha.

Wakaazi wakiangalia mabaki ya nyumba zao yaliounguzwa wakati wa mapigano

Wakaazi wakiangalia mabaki ya nyumba zao yaliounguzwa wakati wa mapigano

Jeshi la polisi tayari limekwisha omba kibali cha mahakama kwa lengo la kufukua kaburi hilo ili kuweza kuhesabu idadi ya miili ya watu iliyozikwa katika kabila hilo. Eric Kiraithe ni msemaji wa wa jeshi la polisi nchini Kenya na Sudi Mnette kwanza alimuuliza wana uhakika kwamba hili kaburi ni la halaiki?

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Mohammed Abdulrahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada