Kuadhibu ugaidi | Matukio ya Kisiasa | DW | 19.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kuadhibu ugaidi

Ujerumani ina azma ya kuimarisha sheria dhidi ya ugaidi.Waziri wa sheria ametangaza vifungu 2 vipya.

Kuanzia wakati gani kuandaa njama za ugaidi kuadhibiwe ? Ujerumani katika vita dhidi ya ugaidi, karibuni hivi itaweza kutumia sheria mpya .Waziri wa sheria wa Ujerumani, bibi Brigitte Zypries, aliujulisha hapo jana mjini Berlin mswada wa sheria mpya za kupambana na ugaidi.Katika kutunga sheria hizo wamelengwa tangu magaidi wa kiislamu wenye itikadi kali hata wale wa siasa kali za mrengo wa kulia.

Ili kukandamiza vitendo vya ugaidi ,serikali huegemea zaidi kifungu cha sheria 129.Kwa muujibu wa kifungu hicho ni kosa kwa yeyote yule anaeunda chama cha kigaidi au anaekiungamkono.Chama hicho lazima kijumlishe si chini ya wanachama 3 ili sheria chini ya klifungu hicho cha 129 iweze kutumika.

Magaidi wenye itikadi kali ya kiislamu wao huchukua muundo tofauti kabisa.Hawajiungi moja kwa moja na jumuiya au kikundi Fulani anadai waziri wa sheria wa ujerumani bibi Zypries na kwahivyo ndio sababu akaona kyafaa kutungwa kifungu kipya cha sheria namba 89.

Kuanzia sasa chini ya kifungu hicho kipya cha sheria itawezekana kuwaadhibu wale wanaoandaa njama ya kgaidi.hapa anakusudia mfano kutoa mafunzo kwenye kambiya magaidi kama nchini Pakistan.Hatahivyo, anaungama waziri huyo wa sheria kutoa ushahidi hapo ni taabu hata kwa matumizi ya sheria hiyo mpya.Anasema bibi Zypries:

“Tunajua kwamba kambi hizo kwa desturi, huanzia awamu ya mafunzo na hasa ya imani za kidini na mazowezi ya kispoti. Hazijishughulishi kabisa na swali:vipi unaweza kutengeza bomu ? Hatuelewi pia wazi,kinapita hasa nini katika kila kambi ya kigaidi.Kwahivyo, lazima pawepo sababu za kutosha zinazoonesha kuwa kwelikuna nia ya kufanya ugaidi.”

Magaidi mfano wa wale 3 waliotiwa mbaroni wiki chache nyuma hapa Ujerumani, wanaweza kupitia vifungu hivi vipya vya sheria kuadhibiwa.

Kwani, wajerumani 2 waliosilimu na mturuki wanatuhumiwa na mshtaki wa serikali kupanga njama ya kuhujumu vituo vya marekani nchini Ujerumani baada ya kupewa mafunzo katika kambi ya kigaidi.

Itabaki si kosa siku zijazo kupata mafunzo Fulani katika kambi ya mafunzo bila ya kuwa na nia ya kufanya ugaidi.

Swali hili kwa jicho la makamo-mwenyekiti wa kundi la wabunge wa chama cha CDU Wolfgang Bosbach,ni kitovu cha sheria hizi mpya.Kwani,kumtilia mtu shaka ana azma ya kutaka kufanya hujuma, ni vigumu kuthibitisha-asema mbunge huyo.

Itakua pia kosa la kuadhibiwa kisheria kutunga mipango ya kufundisha vipi kutengeza silaha au vipi kuandaa hujuma.Mfano halisi hapa anaoueleza waziri wa sheria bibi Zypreis ni maelezo ndani ya mtandao wa Internet juu ya jinsi ya kuunda bomu.

Hapo hakusudii waziri wa sheria Bibi Zypries mwanafunzi ambae kwa ajili ya masomo ya kikemia amefanya taftishi katika mtandao wa maelezo Fulani .Pia hawatadhibiwa chini ya sheria hii, polisi wanasayansi na watafiti.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com