Korea ya Kaskazini kuwekewa vikwazo zaidi? | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 11.06.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Korea ya Kaskazini kuwekewa vikwazo zaidi?

Wanachama wa kudumu kwenye Baraza la Usalama wakubaliana juu ya vikwazo zaidi dhidi ya Korea ya Kaskazini.

Baraza la Usalama latafakari vikwazo zaidi dhidi ya Korea ya Kaskazini.

Baraza la Usalama latafakari vikwazo zaidi dhidi ya Korea ya Kaskazini.

NEW YORK.

Nchi za magharibi zimekubaliana na madola muhimu yanayoiunga mkono Korea ya Kaskazini juu ya kuiwekea nchi hiyo ya kikomunisti vikwazo zaidi katika sekta za silaha na fedha. Nchi hizo pia zimekubaliana juu ya uwezekano wa kuzikagua meli za Korea ya Kaskazini.

Hatahivyo mswada wa azimio la Umoja wa Mataifa juu ya vikwazo hivyo unapaswa kuidhinishwa na Baraza la Usalama.

Lengo la azimio hilo ni kuizuia Korea ya Kaskazini kupata na kuuza nyenzo na tekinolojia ya kuunda silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu.

Azimio hilo pia litawezesha kuizuia Korea ya Kaskazini kupata fedha za kugharamia mipango yake ya silaha.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice amewasilisha mswada wa azimio hilo kwenye Baraza la Usalama ,ambao amesema kuwa ni jibu la kufaa ,kufuatia jaribio la pili la silaha za nyuklia lililofanywa na Korea ya Kaskazini.Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com