1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Kongo yawashtaki wanajeshi waliokiuka haki za binadamu

4 Septemba 2023

Serikali Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, imeamuru kukamatwa mara moja kwa baadhi ya viongozi wa kijeshi kwa kukiuka maagizo na haki za binadamu na kusababisha watu kadhaa kuuwawa.

https://p.dw.com/p/4Vwg1
Demokratische Republik Kongo Gericht Symbolbild
Picha: Pond5/IMAGO

Agizo hilo limetolewa baada ya watu zaidi ya arobaini kuuawa mjini Goma wakati wa maandamano dhidi ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, MONUSCO, ambapo inadaiwa kwamba waliowaua ni askari wa vikosi vya Kongo.

Naibu Waziri Mkuu wa Ulinzi wa Kitaifa pamoja na Waziri wa Haki za Binadamu na Sheria wakiwa katika ziara mjini Goma wamesema wanachunguza hali na watawachukulia hatua baadhi ya viongozi wa kijeshi.

Soma pia:Zaidi ya watu 40 wahofiwa kufariki katika maandamano mjini Goma, Mashariki mwa Kongo

Naibu Waziri Mkuu wa Ulinzi wa Kitaifa Peter Kazidi alisema katika uchunguzi wa awali walifanya mahojiano na maafisa wa jeshi katika eneo husika, na tayari hatua zimechukuliwa kwa wote waliohusika ikiwemo maafisa wa jeshi.

"Kufuatia maagizo ya rais, maafisa kadhaa wa jeshi na polisi wamepelekwa kwenye opfisi ya mashtaka." Alisema

Hata hivyo licha ya serikali kuchukua hatua hizo za kisheria, baadhi ya wananchi wameonesha kutoamini kauli za kisiasa na badala yake wameendelea kulaani hadharani vitendo vya maafisa wa jeshi walivyoyitaja ni kinyume na haki za binadamu.

Baadhi ya raia wameviambia vyombo vya habari kwamba, wahusika halisi bado hawajafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mashirika ya kiraia yataka uchunguzi ukamilike

Mashirika ya kiraia katika jimbo la Kivu Kaskazini yanaunga mkono uamuzi huu wa mamlaka na kuwataka wananchi wa Goma na Kivu Kaskazini kuwa na subira hadi uchunguzi ukamilike.

Masaibu ya wakimbizi wa ndani jimboni Ituri Kongo

Placide Nzilamba ni Rais wa asasi za kiraia za Kivu Kaskazini akizungumza na DW amesema, hatua hiyo ni muhimu katika kusaka haki na kuleta utulivu katika eneo hilo.

Soma pia:Watu wasiopungua kumi wauawa katika maandamano mjini Goma

Katika kuwaenzi wale waliopoteza maisha kwenye mkasa huo, siku ya leo shughuli za kiuchumi zimesimamishwa ikiwa ni ishara ya kuheshimu mchango kwa waliopoteza maisha wakati wanapigania kile walichokiita maslahi ya Goma.